CCM Tanga yanusa harufu ya rushwa kwenye miradi
Автор: Mwananchi Digital
Загружено: 2024-09-29
Просмотров: 329
Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Tanga kimeiagiza Serikali ya mkoa huo, kuchunguza miradi ya maendeleo kwa madai ya kuwapo kuna dalili za rushwa, na kuwachukulia hatua watakaobainika kuhusika.
Agizo hilo limetolewa leo Jumapili Septemba 29, 2024 na Mwenyekiti wa CCM mkoani Tanga, Rajabu Abdallah, wakati akifungua kikao cha kupokea taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025 kwa kipindi cha miezi sita na kusema kuwa katika ziara za ukaguzi miradi waliofanya wamebaini ipo mingine yenye harufu ya rushwa.
Amesema baadhi ya taarifa ambazo walipewa kwenye ukaguzi wa miradi ya afya na elimu waliyopita kuna maeneo mwongozo wa Serikali wa ujenzi umekiukwa na fedha zimekwisha kabla mradi husika kukamilika, hivyo lazima ufuatiliaji ufanyike.
Akitoa taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya CCM Mkuu wa mkoa huo, Balozi Batilda Burian amesema tayari wamefuatilia baadhi ya miradi na kubaini changamoto mbalimbali.
Imeandikwa na Rajabu Athumani
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: