DC MWANZIVA AITAKA CWT MKOA WA LINDI KUWASILISHA KERO ZAO KWA NJIA YA MAJADILIANO NA SI MALALAMIKO.
Автор: Kimeza Production
Загружено: 2025-04-26
Просмотров: 88
Chama cha walimu Tanzania CWT mkoa wa Lindi kimetakiwa kuacha tabia ya kuwasilisha matatizo yao kwa njia isiyo rasmi ya malalamiko na badala yake wametakiwa kujenga hoja na kuandaa mpango kazi wa suluhisho la matatizo yao ambayo watayapaleka katika mamlaka husika ili kupatiwa ufumbuzi wa kudumu.
Hayo yamesemwa na mkuu wa wilaya ya Lindi MH. VICTORIA MWANZIVA alipokua akimwakilisha mkuu wa mkoa wa Lindi MH. ZAINAB TELACK katika mkutano mkuu wa uchaguzi wa Chama cha walimu CWT mkoa uliofanyika katika manispaa ya Lindi.
Awali akisoma risala mbele ya mgeni rasmi katibu wa CWT mkoa wa Lindi SEKELA SIMON licha ya kuishukuru serikali lakini hakusita kueleza changamoto zinazowakabili walimu.
Kisha mkutano huo ukaingia katika agenda ya uchaguzi na hapa MWL. HALIMA LIVETA anatangazwa kuwa mwenyekiti wa CWT mkoa wa Lindi akiitetea nafasi yake kwa kipindi kingine cha miaka mitano.
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: