Ubunifu wa Benki ya Mkombozi kuwahudumia wajasiriamali wadogowadogo wazaa matunda
Автор: Mwananchi Digital
Загружено: 2023-06-26
Просмотров: 143
Benki ya Biashara Mkombozi ilitangaza faida ya Sh 6.79 bilioni kwa mwaka 2022, ambayo ni matokeo mazuri ukilininganisha na kipindi cha nyuma. Benki iliweza kupunguza mikopo chechefu kutoka asilimia 20 mwaka 2020 hadi asilimia 9 kwa mwaka 2022, ikiwa ni kati ya mafanikio makubwa katika kipindi hicho. Thamani za Benki zilikuua kutoa Sh 210 bilioni hadi sh 221 billioni kwa mwaka 2022.
Mafanikio haya yalichangiwa na uimarishaji wa vyanzo vya mapato, kuainisha gharama za uendeshaji wa Benki kwa kuweka mikakati ya kupunguza gharama zisizo na msingi na pia kuthamini muundo wa biashara kwa kuwekeza kwenye huduma za kidigitali ambazo ni Mkombozi Mobile, Internet Banking na Mkombozi Wakala. Benki kwa sasa ina mawakala zaidi ya 400 nchini.
Katika mahojiano na Mwananchi Digital, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Mkombozi, Bw. Respige Kimati, ilieleza namna ubunifu wa kuwahudumia wajasiriamali wadogowadogo ulivyozaa matunda.
Amesema mafanikio hayo yanaashiria dhamira yao ya kutambua na kuhudumia kundi kubwa la watanzania walioinje ya mfumo rasmi wa kifedha.
Amesema wamefanikiwa kubuni programu za kidigitali, lengo likiwa ni kuwafikia wateja wengi zaidi hususan wa chini kabisa, kupanua huduma zaidi kwa kuongeza matawi mapya maeneo tofauti nchini. “Benki ya Mkombozi itajikita katika kuwapa wajisiriamali wa kati na wa chini mikopo inayoendana na mazingira yao halisi ili kukuza biashara na uwezo wa kila mmoja,” amesema Bwana Kimati.
Amesema wanatoa mikopo kwa wajasiriamali waliopo kwenye vikundi ambao wana uwezo wa kukopeshwa kuanzia kiasi cha Sh300,000 hadi Sh4 milioni na kwamba hadi kufikia mwishoni mwa mwaka jana, benki hiyo ilikuwa imeshatoa kiasi cha Sh5.8 bilioni. Kwa ujumla, Benki ya Mkombozi ilitoa kiasi cha Sh115 bilioni kama mikopo mwaka jana, ikiwa ni ongezeko kutoka Sh106 bilioni.
Aidha Kimati amesisitiza umuhimu wa kuweka mazingira bora ya kisera kama vile utoaji wa leseni ili kuwavutia wajasiriamali wengi kuingia katika mfumo rasmi. Amesema Benki ya Mkombozi itazidi kutoa mafunzo mbalimbali kuinua uwezo wa wateja wake kuendesha biashara yao kwa ufanisi.
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: