TABORA WASHEREHEKEA KIZALENDO BIRTHDAY YA RAIS SAMIA
Автор: Daily News Digital
Загружено: 2026-01-27
Просмотров: 60
TABORA: CHUO cha Nyuki mkoani Tabora kimeshiriki pamoja na Watanzania wengine kuadhimisha kumbukizi ya siku ya kuzaliwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kupanda miti ya kivuli na mbao zaidi ya 500 katika Shule ya Sekondari Kariakoo, iliyopo Halmashauri ya Manispaa ya Tabora hatua inayolenga kuboresha mazingira ya shule na kutoa elimu ya vitendo kwa wanafunzi kuhusu uhifadhi wa mazingira. .
Akizungumza wakati wa zoezi hilo, Semu Daud ambae ni mkuu wa Chuo hicho amesema licha ya kuwa na utamaduni wa kupanda miti kila mwaka lakini kuadhimisha kumbukizi ya siku ya kuzaliwa kwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kupitia upandaji miti ni sehemu ya kuunga mkono jitihada za serikali katika kulinda na kuhifadhi mazingira, pamoja na kuhamasisha jamii kushiriki katika shughuli za maendeleo endelevu.
Follow us on:
FACEBOOK;
SpotiLeo: / spotileo-176. .
HabariLeo: / habarileo
DailyNews: / dailynewstz
INSTAGRAM;
HabariLeo: https://instagram.com/habarileo_tz?ig...
SpotiLeo: https://instagram.com/spotileo?igshid...
TWITTER;
Twitter HabariLeo: https://twitter.com/HabariLeo?s=09
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: