WAZIRI MBARAWA AKAGUA UJENZI WA MATANKI YA KUHIFADHI MAFUTA KIGAMBONI
Автор: Millard Ayo
Загружено: 2025-11-27
Просмотров: 2537
Waziri wa Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa ameitaka Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) kutumia muda mwingi kusimamia mradi wa ujenzi wa matanki 15 ya mafuta yenye ujazo wa m³ 380,000.
Amesema kukamilika kwa mradi huo unajengwa kwa fedha za ndani Sh bilioni 703 kutaiwezesha Tanzania kuwa na mafuta ya kutosha pamoja na kuwa na uhakikia wa usalama wa mafuta kwa sababu yatakuwa yanahifadhiwa nchini.
Mbarawa alieleza hayo jana wakati alipofanya ziara kwenye mradi wa ujenzi wa matenki ya kuhifadhia mafuta uliopo Kigamboni Dar es Salaam ambao kwa sasa umefikia asilimia 33. 5.
"Mradi huu ukikamilika utapunguza gharama za maisha na mafuta na utaongeza ufanisi wa bandari kutelemsha mafuta kutoka siku saba hadi hadi chini ya nne," alisema Profesa Mbarawa.
Katika mradi huo matanki sita yatahifadhi mafuta ya dizeli,matano petroli,matenki matatu yatahifadhi mafuta ya ndenge na tenki moja litatumika kama njia ya kusafirishia mafuta kutoka tenki moja kwenda jingine.
Alisema mradi huo ulianza kutekelezwa Agosti mwaka 2024 na unatarajiwa kukamilika Agosti mwaka 2026.
Alieleza kuwa kwa sasa meli ikikaa nangani kila siku mwenye mafuta anachaji Sh milioni 57 kwa hiyo akikaa siku 20 ni karibu Sh milioni 500 gharama hizo hazibaki kwa anayeleta mafuta bali hata kwa watumiaji wa mafuta.
Alimshukuru Rais Samia kwa kuwa na maono ya kuanzisha na kukamilisha miradi mikubwa ya maendeleo ambayo itachochea uchumi wa nchi na kuleta unafuu wa gharama za maisha kwa Watanzania.
Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania, Dk Baraka Mdima alisema kwa ujumla maendeleo ya mradi kwa sasa yanahusisha kukamilika kwa maandalizi ya awali.
Alisema maandalizi ya awali tayari na sasa mradi unaendelea huku akisema wanaendelea sehemu iliyobakia ili kukamilika kwa wakati ulio kwenye mkataba.
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: