Dedication song to JOEL&MARY by Enock Zabron.
Автор: Enock Zabron Mahega
Загружено: 2022-06-05
Просмотров: 2340
PR JOEL E NDEGEA ni rafiki wa pekee ambaye nilibahatika kufahamiana naye mara ya kwanza tukiwa katika ofisi ya msaidizi wa mkuu wa shule Pugu Sekondari mwaka 2013.Katika mazungumzo yake na mwalimu huyo niligundua tabia ya fulani kutoka kwake.Tabia ya kung'ang'ania jambo mpaka litokee.Nilikuja kugundua tabia hiyo kadri nilivyoendelea kumfahamu.
Tulijiunga na masomo ya advance katika shule hiyo ya Pugu na kubahatika kushiriki pamoja katika huduma za kiroho kwa njia ya uimbaji katika kikundi cha YUHAI.Baada ya kumaliza masomo yetu Mungu alijalia tukafaulu na kuchaguliwa kujiunga na chuo kimoja cha MUHIMBILI ambapo tuliishi kwa miaka mingine minne.Hapa nilijifunza mambo makubwa kutoka kwake.Ustahimilivu,kujali kusiko kawaida,utu kwa watu,kutokukata tamaa,ubunifu na mwenye bidii katika kazi.
Alipomaliza masomo yake alifanikiwa kuendelea na majukumu mengine ya maisha lakini katikati ya majukumu hayo akiwa amejaa ndoto kubwa sana za elimu yake,wito kwa kazi ya Mungu ulianza kuingia.Akiwa na maswali mengi na kukataa kwingi,mara kadhaa alinishirikisha anavyojisikia lakini pamoja na hayo alielekeza mawazo yake kwa Mungu kutaka kujua hatima ya wito wa Kichungaji.
Huku akizungumza na watumishi wa Mungu akiomba msaada juu ya wito huo.Mungu aliuzidisha moto huo ndani yake.Hatimaye aliitikia wito akikubali kuongozwa na Bwana.
Ndipo niliwiwa kutunga kiitikio hiki nikimwombea kwaajili ya kazo anayoiendea yeye na mwenzi wake MARY.
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: