Agizo la Rais Magufuli laanza kutekelezwa wilayani Ukerewe
Автор: WazoHuru Media
Загружено: 2018-11-17
Просмотров: 1690
Na George Binagi-GB Pazzo
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Selemani Jafo leo Novemba 17, 2018 amezindua rasmi ujenzi wa miundombinu katika Kituo cha Afya Bwisya kilichopo Ukarawa wilayani Ukerewe.
Mhe. Jafo ameambatana na mwenyeji wake Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhe. John Mongella ambapo ametoa muda wa siku 90 kuanzia leo ujenzi huo uwe umekamilika.
Ujenzi huo unatekelezwa na kampuni ya SUMA JKT chini ya usimamizi wa Kamati Maalum iliyoundwa na Mhe. Mongella kwa gharama ya zaidi ya shilingi milioni 800.
Huu ni utekelezaji wa agizo la Mhe. Rais Dkt. John Magufuli kwamba sehemu ya fedha za rambirambi zilizopatikana kufuatia ajali ya Kivuko cha MV. Nyerere zitumike kufanya ukarabati katika Kituo cha Afya Bwisya ili kuboresha huduma za afya kwa wakazi wa kisiwa cha Ukara.
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: