KIJITONYAMA LUTHERAN CHURCH : IBADA YA EVENING GLORY - THE SCHOOL OF HEALING 19/01/2026
Автор: KIJITONYAMA LUTHERAN CHURCH
Загружено: 2026-01-20
Просмотров: 2777
KIJITONYAMA LUTHERAN CHURCH : IBADA YA EVENING GLORY - THE SCHOOL OF HEALING 19/01/2026
UJUMBE WA LEO: SIRI ILIYOMO NDANI YA UPAKO MPYA
(THE MYSTERY WITHIN THE FRESH ANOINTING)
Ni kukupa Siri zilizojificha ndani ya upako mpya ili uweze kufanikiwa kimaisha
Siri maana yake nini ?
Siri ni jambo (au fumbo) lililofichika machoni pa watu wengi.
Mathayo 13 : 11
11 Akajibu, akawaambia, Ninyi mmejaliwa kuzijua siri za ufalme wa mbinguni, bali wao hawakujaliwa.
Upako maana yake nini?
Neno Upako lina maanisha kupakwa mafuta.
Zaburi 92 : 10
10 Bali pembe yangu umeiinua kama pembe ya nyati, Nimepakwa mafuta mabichi.
Neno Upako katika Agano la kale lilikuwa lina maanisha, Kuwatakasa watu na kutengwa kwa ajili ya kusudi fulani la Mungu.
Kutoka 30 : 30
30 Nawe utawatia mafuta Haruni na wanawe, na kuwatakasa, ili wanitumikie katika kazi ya ukuhani.
Isaya 61 : 1 - 2
1 Roho ya Bwana MUNGU i juu yangu; kwa sababu Bwana amenitia mafuta niwahubiri wanyenyekevu habari njema; amenituma ili kuwaganga waliovunjika moyo, kuwatangazia mateka uhuru wao, na hao waliofungwa habari za kufunguliwa kwao.
2 Kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa, na siku ya kisasi cha Mungu wetu; kuwafariji wote waliao;
Neno Upako katika Agano jipya lina maanisha Nguvu za Roho Mtakatifu.
Matendo 1 : 8
8 Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi.
SIRI YA KWANZA ILIYOPO NDANI YA UPAKO NI KUVUNJA NIRA
Isaya 10 : 27
27 Tena itakuwa katika siku hiyo mzigo wake utaondoka begani mwako, na nira yake shingoni mwako, nayo nira itaharibiwa, kwa sababu ya kutiwa mafuta.
Matendo 10 : 38
38 habari za Yesu wa Nazareti, jinsi Mungu alivyomtia mafuta kwa Roho Mtakatifu na nguvu naye akazunguka huko na huko, akitenda kazi njema na kuponya wote walioonewa na Ibilisi; kwa maana Mungu alikuwa pamoja naye.
Kiroho ina maanisha mateso, uzito unavyomkandamiza mtu asiweze kuwa na uhuru.
Nira kwa lugha nyepesi ni kifungo.
Kuna nira za ulevi , uzinzi, magonjwa, nira za umaskini.
Leo hii, kila nira itavunjika kwa jina la Yesu Kristo.
Mhubiri: Mwl. Davidney Kaale
Kwa maombi na ushauri :
Mch. Kiongozi: Dr. Eliona Kimaro
Simu: +255 655 516 053, +255 754 516 053
Mch. Msaidizi: Anna Kuyonga
Simu: +255 713 553 443
YouTube: Kijitonyama Lutheran church
Barua Pepe : Kijitonyamalutheran@gmail.com
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: