KIJITONYAMA LUTHERAN CHURCH : IBADA YA MORNING GLORY - THE SCHOOL OF HEALING 19/01/2026
Автор: KIJITONYAMA LUTHERAN CHURCH
Загружено: 2026-01-18
Просмотров: 6475
KIJITONYAMA LUTHERAN CHURCH : IBADA YA MORNING GLORY - THE SCHOOL OF HEALING 19/01/2026
UJUMBE WA LEO: MAMBO YA KUOMBEA KATIKA MSIMU MPYA
(PRAYER PRIORITIES FOR A NEW SEASON)
Muhubiri 3 : 1
LENGO LA SOMO
ni kukufahamisha maeneo muhimu ya kuombea katika msimu wako mpya ili uimarishe mahusiano yako na Mungu na ufanikiwe kimaisha.
Msimu mpya maana yake nini kibiblia ni kipindi kipya au majira mpya au ni nyakati mpya ambazo hujawahi kuziishi.
Msimu mpya ni majira mapya yaliyowekwa kwa kusudi maalumu la kiungu
Jambo la kwanza la kuombea ni hili Usiache kumwombea mtu ambaye Mungu amemtuma kukusaidia unapoingia katika msimu wako mpya
Kuna watu ambao Mungu huwainua kwa ajili ya kuwasaidia watu wengine kwenye vipindi mbali mbali vya maisha
Watu wa jinsi hii Mungu huwa anawakutanaisha na wahusika katika wakati upasao.
Esta 3 : 7
7 Basi mwezi wa kwanza, ndio mwezi wa Nisani, mwaka wa kumi na mbili wa mfalme Ahasuero, wakapiga Puri, yaani kura, mbele yake Hamani; siku kwa siku, na mwezi kwa mwezi, hata mwezi wa kumi na mbili, ndio mwezi wa Adari.
Watu waliopewa jukumu la mamma hii kama Esta wanatakiwa kuombewa sana.
Esta 4 : 15 - 16
15 Basi Esta akawatuma ili wamjibu Mordekai,
16 Uende ukawakusanye Wayahudi wote waliopo hapa Shushani, mkafunge kwa ajili yangu; msile wala kunywa muda wa siku tatu, usiku wala mchana, nami na wajakazi wangu tutafunga vile vile; kisha nitaingia kwa mfalme, kinyume cha sheria; nami nikiangamia, na niangamie.
Zaburi 105 : 16 - 21
16 Akaiita njaa iijilie nchi, Akakiharibu chakula chote walichokitegemea.
17 Alimpeleka mtu mbele yao, Yusufu aliuzwa utumwani.
18 Walimwumiza miguu yake kwa pingu, Akatiwa katika minyororo ya chuma.
19 Hata wakati wa kuwadia neno lake, Ahadi ya Bwana ilimjaribu.
20 Mfalme alituma watu akamfungua, Mkuu wa watu akamwachia.
21 Akamweka kuwa bwana wa nyumba yake, Na mwenye amri juu ya mali zake zote.
Ndugu za Yusufu hawakujua Yusufu ametumwa na Mungu kuwasaidia katika kipindi cha miaka saba.
Yusufu alitumwa na Mungu kwa ajili ya kuwasaidia waebrania, Wamisri na dunia ya kipindi kile.
Mungu akutumie Yusufu wako atakae kuvusha katika msimu mpya uliopo.
Mhubiri: Mwl. Davidney Kaale
Kwa maombi na ushauri :
Mch. Kiongozi: Dr. Eliona Kimaro
Simu: +255 655 516 053, +255 754 516 053
Mch. Msaidizi: Anna Kuyonga
Simu: +255 713 553 443
YouTube: Kijitonyama Lutheran church
Barua Pepe : Kijitonyamalutheran@gmail.com
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: