MAHAFALI YA 23 YA TAASISI YA UHASIBU TANZANIA T.I.A NA YA KUMI NA MOJA KWA KAMPASI YA KIGOMA-2025
Автор: Main FM Tanzania
Загружено: 2025-11-23
Просмотров: 125
Novemba 21, 2025 mkoa wa Kigoma unashuhudia historia ikiandikwa katika Mahafali ya 23 ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania T.I.A ambayo ni ya 11 katika Kampasi ya Kigoma na kwa mara ya kwanza yakifanyikia katika Majengo mapya ya Kampasi hii yaliyoko eneo la Kamara kata ya Mngonya Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma.
Takribani Wahitimu 757 kutoka ngazi tofauti tofauti katika mahafali haya wanatarajiwa kutunukiwa vyeti na mgeni rasmi katika mahafali haya ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Kigoma IGP Mstaafu Balozi Simon Nyakoro Sirro.
Ni mahafali ya Kihistoria huku Historia ya mahafali haya ikichagizwa na mahafali haya kufanyika kwa mara ya kwanza katika majengo mapya ya Kampasi hii yaliyoko eneo la Kamara kata ya Mngonya Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma.
Majengo haya ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa majengo ya kudumu ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) Kampasi ya Kigoma ambao unagharimu takribani Tsh. Bilioni 11 Milioni 80 na Laki 7 Thelatini na Tano Elfu na 67 ambao mpaka hivi sasa umefikia 90% ya utekelezwaji wake.
Profesa William Palangyo ni Afisa Mtendaji mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) na kupitia mahafali haya, hapa anaeleza sehemu ya mradi huu ulipofikia na sehemu ya majengo yanayopatikana katika mradi huu.....
Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) Kampasi ya Kigoma imeendelea kujikita katika kutoa elimu kwa kuzingatia maendeleo ya soko la ajira pamoja na ujuzi stahiki......
Pamoja nayo pia imeendelea kujidhatiti katika kutoa ushauri wa kitaalamu kwa wafanyabiashara wa Kigoma katika nyanja za Biashara, Rasilimali watu, Masoko na Uhasibu kama ambavyo anaeleza Profesa William Palangyo........
Mgeni rasmi katika mahafali haya Mkuu wa mkoa wa Kigoma IGP Mstaafu Balozi Simon Nyakoro Sirro ameipongeza Menejimenti ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) kwa namna inavyosimamia utekelezwaji wa mradi huu, pamoja nayo ameipongeza Serikali ya awamu ya Sita kwa kuridhia kutoa kiasi hicho cha fedha kwa ajili ya utekelezwaji wa mradi huu wa maeneo ya kudumu ya TIA Kampasi ya Kigoma.
Akizungumza na Wahitimu Balozi Simon Sirro amewataka vijana kujibidiisha katika matumizi ya Teknolojia kuongeza ubunifu ili kukimbizana na kasi ya mabadiliko ya kidigitali yanayotokea ulimwenguni ikiwa ni pamoja na matumizi ya Akili Mnemba........
Kwa kuthibitisha ubora wa Elimu pamoja na ujuzi mbalimbali ambao unatolewa na Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) kampasi ya Kigoma, Ezekiel Kasika huyu ni mwanafunzi shahada ya Manunuzi na Ugavi na hapa anaelezea namna Elimu aliyoipata kutoka Taasisi ya Uhasibu Tanzania TIA pamoja na ujuzi namna ilivyomsaidia kuja na ubunifu huu wa kubuni Website.....
SUBSCRIBE NOW NA BONYEZA ALAMA YA KENGELE🔔 UWE WA KWANZA KUONA👉 / @mainfmtanzania
KIGOMA========KASULU========UVINZA======BUHIGWE========KIBONDO==============BURUNDI================ ⚫️ WASILIANA NA MAIN FM RADIO : ( +255 677 775 533), ⚫️ Email: [email protected] ⚫️ OUR PLAYLISTS: ⚫️ MICHEZO na BURUDANI: / @mainfmtanzania ⚫️ MAKALA ZA KUSISISIMUA ⚫️ LIVE VIPINDI VYA RADIO: / @mainfmtanzania ⚫️ EXCLUSIVE INTERVIEW: • UTACHEKA MANENO YA SHOMBO YA SUDA YANGA | ... ⚫️ SIKILIZA MAIN FM RADIO LIVE : https://mainfm.co.tz/ ⚫️ Kwa UPDATES zote, Tufollow
Instgram: https://www.instagram.com/mainfmtanza...
Facebook: https://www.facebook.com/watch/?v=168...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: