Популярное

Музыка Кино и Анимация Автомобили Животные Спорт Путешествия Игры Юмор

Интересные видео

2025 Сериалы Трейлеры Новости Как сделать Видеоуроки Diy своими руками

Топ запросов

смотреть а4 schoolboy runaway турецкий сериал смотреть мультфильмы эдисон
dTub
Скачать

Maumivu ya kichwa kwa Mjamzito | Mama Mjamzito kuumwa Kichwa!

Автор: Dr. Mwanyika

Загружено: 2020-10-06

Просмотров: 38937

Описание:

Kuumwa kichwa kwa Mama Mjamzito huweza kutokea kwa sababu ya mabadiliko ya kibaolojia katika mwili wa Mama huyo.

Lakini kumbuka kwamba wanawake ambao wana umri ambao wanaweza kubeba Mimba ndio huongoza kuwa na maumivu ya kichwa kuliko Wanaume,Wanawake baadhi hupata maumivu ya kichwa kutoka(Kipanda uso) kwa sababu ya kubadilika badilika kwa homoni katika mizunguko yao ya siku au Hedhi!

Mama Mjamzito kama unapata maumivu ya kichwa jiulize maswali haya hapa chini!

Swali la 1. Je umekuwa na maumivu katika vipindi fulani fulani tokea angali huna Mimba na maumivu bado yanatokea vile vile bila mabadiliko?

Swali la 2. Je umekuwa na maumivu kwa Mara ya kwanza wakati wa Ujauzito?

Swali la 3. Je ulikuwa na maumivu tokea huna ujauzito na kwa sasa maumivu yamekuwa makali zaidi au yamebadilika na kuwa zaidi?

Swali la 2 na swali la 3 ni maswali muhimu sana kwa sababu kama unapata maumivu hayo, inawezekana una shida fulani naomba soma hapa chini, yawezekana maumivu hayo ni kutoka na sababu hizi👇👇👇👇!

1. Maumivu kutoka na shida ya kichwa chenyewe:
Maumivu haya hutokana na shida zifuatazo;

A.KIPANDA USO( MIGRAINE HEADACHE).
Dalili zake;
Maumivu ya kichwa upande mmoja wa kichwa,
Maumivu ya kupwita pwita,
Kupata shida kuona huweza kuambatana na kutapika na kichefu chefu.

MUHIMU;Ukiona dalili hizo kama ni mjamzito wahi hospitali usinunue dawa kiholela.

B. CLUSTER HEADACHE
Dalili zake;
Maumivu kwenye eneo la jicho moja au sehemu ya juu ya jicho Mara nyingi huwa ni upande mmoja wa kichwa na huwa ya kupwita pwita.

MUHIMU; Ili kupinguza maumivu hayo pata hewa safi ya Oksjeni na wahi Hospitali.

C. TENSION TYPE HEADACHE
Dalili zake;
Maumivu huwa pande mbili za kichwa au kichwa chote huwa kama yanabana ukiona dalili hizo wahi hospitali.

2. Maumivu ya kichwa kutokana na magonjwa mengine yanaweza kuwa ya kuambukizwa au yasiyoambukizwa.
Kwa mama mjamzito yanaweza kutokana na Magonjwa kama;
Kiharusi,kupasuka au kuziba kwa mishipa ya damu kichwani au kwenye ubongo,presha wakati wa ujauzito au dalili za kifafa cha Mimba!

MUHIMU; Presha wakati wa Mimba!,
Endapo umepata maumivu ya kichwa kuanzia wiki 20 au miezi 5 ya Mimba kwenda juu mpaka Wiki 4 Mara baada ya kujifungua,

Maumivu hayo huweza kuwa ya ghafla au huja kidogo kidogo na makali zaidi,

Haya pungui kwa dawa za maumivu,

Huuma sehemu ya nyuma ya kichwa au sehemu ya mbele au kichwa chote lakini pia inawezekana yanaambata na kuvimba kwa uso, miguu na mikono au mwili kiujumla.

Lakini pia huweza kuhusisha kupata shida ya kuona.

MUHIMU; Unatakiwa kuwahi hospitali mapema kupatiwa matibabu kwa sababu yaweza kuwa una presha ya Mimba au dalili za mwanzo za kifafa cha Mimba!

Kwa nini ni muhimu kutibu Maumivu ya kichwa sababu kama usipotibu maumivu ya kichwa yatakupa msongo wa mawazo,kuto kula vizuri,kukosa usingizi na kutojisikia vizuri hii huweza kuathiri ukuaji wa mtoto wako tumboni.

Mara ya kutibu Maumivu ya kichwa hakikisha unaacha na tabia hatarishi za kukusababisha kupata maumivu ya kichwa kwa kuhakikisha unapata usingizi wa kutosha,Fanya mazoezi, usiwe unaacha baadhi ya muda kula chakula na badili mtindo wako wa maisha pia!

NB: Ukitaka kujifunza zaidi ni fuatilie YouTube kwa jina la Dr.Mwanyika au bonyeza link hapo 👇👇👇👇
   / drmwanyika  

Ukiwa unamaswali unaweza kuuliza hapa chini (kwenye comments za youtube).

Subscribe,Comment and Share

JapideAfya_Services
Your Health is Our Health
Instagram as @JapideAfya_Services
Facebook page as @JapideAfya_Services
©Dr.Mwanyika.

#MamaAfya
#MaumivuKichwa
#Ujauzito

Maumivu ya kichwa kwa Mjamzito | Mama Mjamzito kuumwa Kichwa!

Поделиться в:

Доступные форматы для скачивания:

Скачать видео mp4

  • Информация по загрузке:

Скачать аудио mp3

Похожие видео

Je Maumivu ya kichwa kwa Mjamzito ktk miezi 3 ya mwanzoni husababishwa na nini? | Kichwa kuuma sana.

Je Maumivu ya kichwa kwa Mjamzito ktk miezi 3 ya mwanzoni husababishwa na nini? | Kichwa kuuma sana.

MEDICOUNTER EPS 10: MAUMIVU YA KICHWA

MEDICOUNTER EPS 10: MAUMIVU YA KICHWA

MAUMIVU YA KICHWA KWA MAMA MJAMZITO | HEADACHE FOR PREGNANT MOTHERS

MAUMIVU YA KICHWA KWA MAMA MJAMZITO | HEADACHE FOR PREGNANT MOTHERS

Je Mtoto Kucheza Miezi 3 ya mwanzoni mwa Ujauzito ni kawaida? {Mtoto kucheza miezi 3 ya mwanzo}!?.

Je Mtoto Kucheza Miezi 3 ya mwanzoni mwa Ujauzito ni kawaida? {Mtoto kucheza miezi 3 ya mwanzo}!?.

JE MAUMIVU UKENI KWA MJAMZITO HUTOKANA NA NINI?? | JINSI YA KUPUNGUZA MAUMIVU UKENI KTK UJAUZITO!!

JE MAUMIVU UKENI KWA MJAMZITO HUTOKANA NA NINI?? | JINSI YA KUPUNGUZA MAUMIVU UKENI KTK UJAUZITO!!

Je Maumivu ya Tumbo ya kubana na kuachia kwa Mjamzito husababishwa na Nini? | Je ni hatari au lah?

Je Maumivu ya Tumbo ya kubana na kuachia kwa Mjamzito husababishwa na Nini? | Je ni hatari au lah?

Dalili za Mimba ya Mtoto wa Kike Tumboni mwa Mjamzito! | Ni zipi Dalili za Mimba ya Mtoto wa Kike??.

Dalili za Mimba ya Mtoto wa Kike Tumboni mwa Mjamzito! | Ni zipi Dalili za Mimba ya Mtoto wa Kike??.

Dalili za Mimba ya Mtoto wa kiume / Je kuna ukweli katika dalili hizi za mtoto wa kiume tumboni????

Dalili za Mimba ya Mtoto wa kiume / Je kuna ukweli katika dalili hizi za mtoto wa kiume tumboni????

Ukiona Dalili hizi jua unakaribia Jifungua,Jiandae - Dr Baiya Kissiwa

Ukiona Dalili hizi jua unakaribia Jifungua,Jiandae - Dr Baiya Kissiwa

Je Mtoto kucheza zaidi Tumboni mwa Mjamzito huwa ni hatari? | Je husababishwa na nini?

Je Mtoto kucheza zaidi Tumboni mwa Mjamzito huwa ni hatari? | Je husababishwa na nini?

ВОССТАНОВЛЕНИЕ НЕРВНОЙ СИСТЕМЫ! Музыка для глубокой души!Музыка, что лечит! Слушай и чувствуй

ВОССТАНОВЛЕНИЕ НЕРВНОЙ СИСТЕМЫ! Музыка для глубокой души!Музыка, что лечит! Слушай и чувствуй

JE KUTOKWA NA UCHAFU MWEUPE UKENI KWA MJAMZITO HUSABABISHWA NA NINI? | SABABU ZA UCHAFU UKENI??.

JE KUTOKWA NA UCHAFU MWEUPE UKENI KWA MJAMZITO HUSABABISHWA NA NINI? | SABABU ZA UCHAFU UKENI??.

SABABU ZA KUVIMBA MIGUU WAKATI WA UJAUZITO

SABABU ZA KUVIMBA MIGUU WAKATI WA UJAUZITO

Dalili za Mimba changa. Zifahamu dalili 10 za uhakika za #mimba changa

Dalili za Mimba changa. Zifahamu dalili 10 za uhakika za #mimba changa

Je ni kwa nini Mapigo ya Moyo kwenda mbio kwa Mjamzito?? | Mapigo ya Moyo kwenda mbio kwa Mjamzito??

Je ni kwa nini Mapigo ya Moyo kwenda mbio kwa Mjamzito?? | Mapigo ya Moyo kwenda mbio kwa Mjamzito??

ПОСЛЕ СМЕРТИ ВАС ВСТРЕТЯТ НЕ РОДСТВЕННИКИ, А.. ЖУТКОЕ ПРИЗНАНИЕ БЕХТЕРЕВОЙ. ПРАВДА КОТОРУЮ СКРЫВАЛИ

ПОСЛЕ СМЕРТИ ВАС ВСТРЕТЯТ НЕ РОДСТВЕННИКИ, А.. ЖУТКОЕ ПРИЗНАНИЕ БЕХТЕРЕВОЙ. ПРАВДА КОТОРУЮ СКРЫВАЛИ

Ukiwa na DALILI hizi 10, fahamu kuwa wewe ni MJAMZITO tayari | Bonge la Afya

Ukiwa na DALILI hizi 10, fahamu kuwa wewe ni MJAMZITO tayari | Bonge la Afya

LIVE# MISA TAKATIFU YA KUFUNGA JUBILEI KUU 2025 NA DARAJA TAKATIFU LA USHEMASI JIMBO LA IRINGA

LIVE# MISA TAKATIFU YA KUFUNGA JUBILEI KUU 2025 NA DARAJA TAKATIFU LA USHEMASI JIMBO LA IRINGA

Если у тебя спросили «Как твои дела?» — НЕ ГОВОРИ! Ты теряешь свою силу | Еврейская мудрость

Если у тебя спросили «Как твои дела?» — НЕ ГОВОРИ! Ты теряешь свою силу | Еврейская мудрость

5 супов, которые омолаживают организм изнутри: советы врача

5 супов, которые омолаживают организм изнутри: советы врача

© 2025 dtub. Все права защищены.

  • Контакты
  • О нас
  • Политика конфиденциальности

Контакты для правообладателей: [email protected]