Популярное

Музыка Кино и Анимация Автомобили Животные Спорт Путешествия Игры Юмор

Интересные видео

2025 Сериалы Трейлеры Новости Как сделать Видеоуроки Diy своими руками

Топ запросов

смотреть а4 schoolboy runaway турецкий сериал смотреть мультфильмы эдисон
dTub
Скачать

WAZIRI WA NISHATI MHE. NDEJEMBI AZINDUA RASMI MITA JANJA

Автор: MISALABA MEDIA

Загружено: 2025-12-05

Просмотров: 33

Описание:

Waziri wa Nishati Mhe. Deogratius Ndejembi amezindua rasmi mita janja (smart meter) yenye lengo la kuboresha na kumrahisishia mteja kufanya manunuzi ya umeme moja kwa moja ikiwa ni mageuzi makubwa ya teknolojia yanayofanywa na TANESCO katika kuongeza ufanisi wa utoaji wa huduma kwa wateja.

Waziri wa Nishati amezindua Mita janja hizo Disemba 05, 2025 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC), na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali, wadau wa sekta ya nishati na watendaji wa TANESCO.

Amesema Mita hizo mpya zinamwezesha mteja kupata umeme mara moja baada ya kufanya manunuzi ya token bila kutumia kifaa cha ziada cha kuingiza namba (CIU), hatua inayolenga kupunguza changamoto zilizokuwa zikijitokeza katika mfumo wa zamani.

“Leo tunajivunia hatua kubwa ya kihistoria zilifanywa na TANESCO ikiwa ni moja ya kampuni za umma inayofanya vizuri katika utoaji huduma kwa wateja nchini. Mita janja inaleta mapinduzi makubwa katika namna Shirika hili linavyofanya usimamizi wa ukusanyaji wa mapato,” ameeleza Mhe. Ndejembi.

Ameongeza kuwa changamoto zilizokuwa zikiwakabili wateja wakati wa kuingiza token ndiyo zimeisukuma Serikali kufanya mageuzi ya kiteknolojia.

“Uzinduzi huu unaweka alama kubwa kwa nchi yetu kwenye mapinduzi ya tekinolojia , hivyo naielekeza TANESCO kuhakikisha inasamabaza mita hizi maeneo yote yenye uhitaji mkuwa na kuhakikisha inaendana na viwango vya kimataifa sambamba na kutoa elimu za faida ya mita hizo,” alisisitiza.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Salome Makamba, amesema uzinduzi wa Mita Janja ni mwendelezo wa dhamira ya Serikali katika kuboresha huduma kwa wananchi.

“Nimefurahi kushuhudia hatua hii kubwa ya mapinduzi, ikiwa ni siku ya 33 tangu Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan aingie madarakani. Leo tunaweka historia muhimu kupitia uzinduzi wa Mita Janja kwa wateja wa TANESCO,” alisema Mhe. Salome.

Naye, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Albert Chalamila, amesisitiza umuhimu wa kulinda miundombinu ya umeme na kupongeza TANESCO kwa kuimarisha ushirikiano na vyombo vya ulinzi na usalama katika kudhibiti vitendo vya uharibifu.

“Hatua hii itukumbushe wajibu mkubwa tulionao kulinda miundombinu. Nawapongeza TANESCO kwa ushirikiano wao na Jeshi la Polisi katika kupambana na uhujumu dhidi ya miundombinu. Endeleeni kwa kasi hii ili huduma ya umeme ipatikane kwa uhakika,” alisema , Mhe. Chalamila.

Aidha, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mha. Felichesmi Mramba, ametoa pongezi kwa TANESCO kwa utekelezaji huu kwa wakati muafaka, akieleza kuwa teknolojia ya Mita Janja itarahisisha kwa kiwango kikubwa utambuzi wa changamoto za wateja kabla ya mteja kutoa taarifa TANESCO.

Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TANESCO, Balozi Zuhura Bundala, alisema Bodi inaona fahari kuona mageuzi yanayoendelea katika uboreshaji wa huduma zinazotolewa na Shirika na kuwa bodi hiyo inazidi kupata moyo katika kuliongoza Shirika kutoa huduma bora zaidi kidigitali.

WAZIRI WA NISHATI MHE. NDEJEMBI AZINDUA RASMI MITA JANJA

Поделиться в:

Доступные форматы для скачивания:

Скачать видео mp4

  • Информация по загрузке:

Скачать аудио mp3

Похожие видео

HAFLA YA UZINDUZI WA MITA JANJA ZA UMEME KWA WATEJA WA TANESCO

HAFLA YA UZINDUZI WA MITA JANJA ZA UMEME KWA WATEJA WA TANESCO

Rais MAGUFULI Alivyowabana TANESCO, Nusura AWATUMBUE!

Rais MAGUFULI Alivyowabana TANESCO, Nusura AWATUMBUE!

WAZIRI MAVUNDE AZUNGUMZA NA WACHIMBAJI MWAKITOLYO, AFAFANUA MSAADA WA KIUFUNDI

WAZIRI MAVUNDE AZUNGUMZA NA WACHIMBAJI MWAKITOLYO, AFAFANUA MSAADA WA KIUFUNDI

Мухаммед Али против Ивана Драго! Этот Бой не Забыть...

Мухаммед Али против Ивана Драго! Этот Бой не Забыть...

Inside the Largest Wood Sawmill Factory – How Plywood Is Made From Logs to Table (Full Process)

Inside the Largest Wood Sawmill Factory – How Plywood Is Made From Logs to Table (Full Process)

TANESCO TABORA YAFANYA MAPINDUZI KWA WATEJA KUUNGANISHIWA UMEME KWA SIMU

TANESCO TABORA YAFANYA MAPINDUZI KWA WATEJA KUUNGANISHIWA UMEME KWA SIMU"WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA"

SHUWASA YATOA SALAMU ZA KRISMAS NA MWAKA MPYA SHINYANGA, TINDE, DIDIA NA ISELAMAGAZI

SHUWASA YATOA SALAMU ZA KRISMAS NA MWAKA MPYA SHINYANGA, TINDE, DIDIA NA ISELAMAGAZI

Путин наградил Михалкова, Захарову, Соловьева, Канделаки, Мацуева, Спивакова и Абдразакова

Путин наградил Михалкова, Захарову, Соловьева, Канделаки, Мацуева, Спивакова и Абдразакова

Китай вскрыл Луну: Что на самом деле нашли на обратной стороне?

Китай вскрыл Луну: Что на самом деле нашли на обратной стороне?

❗️❗️ Зеленский назвал 20 пунктов мирного плана | Оперативные новости. День

❗️❗️ Зеленский назвал 20 пунктов мирного плана | Оперативные новости. День

TANESCO WAKAMATA WIZI WA UMEME  UNAOFANYIKA KWENYE JUMBA HILI LA KIFAHALI BAGAMOYO

TANESCO WAKAMATA WIZI WA UMEME UNAOFANYIKA KWENYE JUMBA HILI LA KIFAHALI BAGAMOYO

2025 MATALAMU NG'WANIKE

2025 MATALAMU NG'WANIKE

MSTAHIKI MEYA MPYA JIJI LA DSM ATOA DIRA YA UONGOZI WAKE

MSTAHIKI MEYA MPYA JIJI LA DSM ATOA DIRA YA UONGOZI WAKE

КТО УБИЛ СССР? ЕЛЬЦИН РАСКРЫЛ ПРАВДУ, КОТОРУЮ СКРЫВАЛИ 35 ЛЕТ!

КТО УБИЛ СССР? ЕЛЬЦИН РАСКРЫЛ ПРАВДУ, КОТОРУЮ СКРЫВАЛИ 35 ЛЕТ!

⚡Россияне, ГОТОВЬТЕСЬ к ужасу в 2026! ПЛОХИЕ НОВОСТИ для всей РФ. Вот что будет @Популярная политика

⚡Россияне, ГОТОВЬТЕСЬ к ужасу в 2026! ПЛОХИЕ НОВОСТИ для всей РФ. Вот что будет @Популярная политика

RC MBONI MHITA AWATAKIA WANANCHI WA SHINYANGA KRISMASI NJEMA, ASISITIZA AMANI, UPENDO NA USALAMA

RC MBONI MHITA AWATAKIA WANANCHI WA SHINYANGA KRISMASI NJEMA, ASISITIZA AMANI, UPENDO NA USALAMA

Քոչարյանի քաղաքական մեհիդը պիտի փռել, Կարապետյանը քաղաքական մարած դեմք է | ԱՆՑՆԵԼՈՎ ՍԱՀՄԱՆԸ

Քոչարյանի քաղաքական մեհիդը պիտի փռել, Կարապետյանը քաղաքական մարած դեմք է | ԱՆՑՆԵԼՈՎ ՍԱՀՄԱՆԸ

Inside a Crunchy Peanut Butter Factory: How They Make the Perfect Crunch | Full Process

Inside a Crunchy Peanut Butter Factory: How They Make the Perfect Crunch | Full Process

⚡Внезапное ЗАЯВЛЕНИЕ США по войне! У Трампа ОШАРАШИЛИ по переговорах. Вот что сказали @ВОТ ЧТО

⚡Внезапное ЗАЯВЛЕНИЕ США по войне! У Трампа ОШАРАШИЛИ по переговорах. Вот что сказали @ВОТ ЧТО

Россия показала «Призрак»:  чем грозит новая ракета соседям Украины. Запад Украины больше не тыл

Россия показала «Призрак»: чем грозит новая ракета соседям Украины. Запад Украины больше не тыл

© 2025 dtub. Все права защищены.

  • Контакты
  • О нас
  • Политика конфиденциальности

Контакты для правообладателей: [email protected]