VIJANA 1,651 WAPATA ELIMU AFUA ZA AFYA YA UZAZI, STADI ZA MAISHA NA UCHUMI ENDELEVU
Автор: Makutano TV
Загружено: 2025-12-19
Просмотров: 69
Kwa mujibu wa Shirika la SOS Children’s villages Iringa, Jumla ya vijana 1851 katika Wilaya ya Mufindi, Mafinga mji na Kilolo Mkoani Iringa wamefikiwa na elimu ya afua za afya ya uzazi, stadi za maisha na Uchumi endelevu kupitia mradi wa Initiatives for Empowering Adolescents (IEA katika kipindi cha Julai hadi Septemba 2025.
Mashujaa wawili kutoka katika Sekta nyeti isiyozungumziwa mara nyingi, tuwatambue vinara hawa wauguzi wanawake, ambao ni wahudumu wa Afya kutoka Zahanati ya Kitelewasi Lungemba, Bi. Fimo Amoni Kihaga muuguzi na mhudumu wa afya, pia kutoka Zahanati ya Mkalala Mufindi ni muuguzi Martha Samuel Kapugi.
Sote tunafahamu kuwa wauguzi wana jukumu muhimu katika huduma za afya na huduma za dharura katika jamii.
Fimo na Martha wamejengewa uwezo juu ya utoaji wa elimu rika na Shirika hili la SOS, na haya ni matokeo baada ya kujengewa uwezo
Initiatives for Empowering Adolescents (IEA) ni mradi uliojikita kuwajengea uwezo vijana katika afua za Afya ya Uzazi, Stadi za Maisha na Uchumi Endelevu kwa mabinti waliopata ujauzito ama watoto katika umri mdogo.
Mradi huu unaotekelezwa mkoani Iringa katika wilaya za Kilolo na Mufindi na Shirika la SOS umejikita katika mtazamo na msingi wa haki na ujumuishi, kwa lengo la kuongeza ufanisi na upatikanaji wa taarifa na huduma za afya ya uzazi kwa vijana wote umejumuisha wauguzi na watoa huduma ngazi ya jamii ili kuhakikisha vijana wanapatiwa maarifa, ujuzi, rasilimali na msaada wanaouhitaji ili kuwasaidia katika kufanya maamuzi sahihi kuhusu afya na ustawi wao.
Kama wanajamii wanaoaminika, wauguzi huweka kielelezo kwa wengine na kuendelea kukuza afya nje ya mahali pao pa kazi. Hata hivyo utafiti ulionyesha kuwa wauguzi mara nyingi hawajipi sifa nyingi kwa michango hii.
Kwa mujibu wa Takwimu za Halmashauri ya Mufindi kwa Mwaka 2024 asilimia 11 ya wasichana chini ya miaka 19 walipata ujauzito na Mafinga Mji ni asilimia 8.6
Ms,TUKUSWIGA MWAISUMBE
Founder Makutano TV
+255 754 298 118/+255 684 298 118
Facebook:Tukuswiga Mwaisumbe
Instagram:tukuswigamwaisumbe4222
You Tube Makutano TV / instagram makutano TV
"Storms do not last Forever"
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: