WASIMAMIZI WA VITUO VYA KUPIGIA KURA NANYAMBA WAELEZA UMUHIMU WA MAFUNZO
Автор: CHIVIHI MEDIA
Загружено: 2025-10-27
Просмотров: 21
Wasimamizi wa vituo vya kupigia kura jimbo la Nanyamba wamhitimisha mafunzo ya siku mbili maalumu kwa ajili ya kusimamia vituo katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika tarehe 29 mwezi Oktoba mwaka huu.
Mafunzo hayo yametolewa na tume huru ya uchaguzi nchini na kufanyika katika shule ya sekondari Nanyamba mkoani Mtwara kuanzia October 27 na 27,2025.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wameeleza kuwa kupitia elimu hiyo itawasidia kutoa huduma kwa wapiga kura na kutoa kipaumbele kwa wenye mahitaji maalumu wakiwemo wazee, walemavu, wajawazito na wanaonyonyesha.
Naye Joseph Mhagama ambaye ni Msimamizi wa uchaguzi wa Jimbo la Nanyamba amewaasa wasimamizi hao kufuata Sheria na taratibu za tume huru ya uchaguzi ili kuondoa malalamiko na vurugu wakati wa uchaguzi.
Tufuate Instagram, TikTok, Facebook na WhatsApp channel @chivuhimedia. Subscribe YouTube channel yetu uwe mjanja na wakwanza kupata habari zetu.
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: