DAY 5 - NOVENA TO THE HOLY SPIRIT (NOVENA YA ROHO MTAKATIFU)
Автор: AMANI MEDIA CATHOLIC TV
Загружено: 2025-06-02
Просмотров: 72
DAY 5 | NOVENA YA ROHO MTAKATIFU|TUNAOMBA ROHO MTAKATIFU AYAGEUZE MAISHA YETU
Welcome to Day 5 of the Novena to the Holy Spirit—the most ancient of all novenas, prayed with the Church in preparation for the great Feast of Pentecost
NOVENA YA ROHO MTAKATIFU
SIKU YA TANO
TUNAOMBA ROHO MTAKATIFU AYAGEUZE MAISHA YETU
Ewe Roho Mtakatifu, upendo na uzuri, uchangamfu,wa Baba na Mwana, maua na harufu ya utakatifu wa Mungu. Moto mtakatifu uliowashwa ndani yangu.
Uufanye moyo wangu uwe mpya, yasafishe madoa yote, ondoa giza, teketeza uchafu wote na uniumbie sura takatifu ya Mwana. Roho unayewaka na upendaye kukaa kwangu pekee ili uweze kunitakatifuza, washa moto huu wa mapendo, uingilie moyo wangu na ujiingize na mwali wako wa moto. Ondoa mambo yote yenye nia mbaya na wenye mipango mibaya. Nipe nguvu ya kuwa mtume awezaye kutekeleza kazi yake. Nipe neema ya kuwa mwali wa moto na uweke kwangu katika hali ya usafi wa moyo na upendo.
Tuombe:
Sifa, utukufu, heshima na upendo ni kwako wewe chanzo cha uzima wa Roho ambaye ametuletea duniani Mwokozi wabRoho zetu. Heshi na utukufu ni kwake yeye ahabudiwe na Moyo utupendao bila mwisho.
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: