WAZIRI MKUU KUZINDUA MELI YA MV NEW MWANZA KESHO
Автор: BONGO PLAY TELEVISION
Загружено: 2026-01-22
Просмотров: 7
Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Mwigulu Nchemba anatarajiwa kuzindua meli ya Mv New Mwanza ambayo tayari ujenzi wake umekamilika
Akizungumzia ziara ya Waziri mkuu mkoani Mwanza waziri wa Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa amesema Dk Mwigulu atazindua rasmi meli hiyo January 23 mwaka huu kwa ajili ya kuanza kuhudumia wanananchi kupitia safari zake
Profesa Mbarawa amesema kuwa meli hiyo imejengwa kisasa na inauwezo mkubwa wa kubeba abiria na mizigo ambapo mpaka kukamilika kwa ujezi wake imegharimu zaidi ya shilingi bilioni 120 huku akiishukuru serikali ya awamu ya 6 kwakutoa fedha za kukamilisha ujenzo huo
Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Mwanza Said Mtanda ametumia nafasi hiyo kutoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi katika maeneo yote akapofika waziri Mkuu kwa ajili ya kumsikiliza
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: