Jinsi ya kuangalia Nyota? au Jinsi ya kuchambua Nyota?
Автор: Rakims Spiritual
Загружено: 2025-04-02
Просмотров: 6820
#nyota #Kuangalianyota
Jinsi ya kuangalia Nyota?
Kwanza kabisa fahamu ya kuwa Nyota ni tawi linalojulikana kwa kiswahili fasaha kama MakundiNyota.
Nayo ni Moja kati ya Elimu ya Sayansi ya kiroho inayofahamika kama Astrology kingereza na kiswahili fasaha huitwa UNAJIMU.
Unajimu ni somo pana sana ambalo katika kipengele cha kusoma unajimu basi huwa Tunaangalia MakundiNyota 12,
Ambayo nayo ni maarufu kwa watu wengi na hutambulika kama elimu ya nyota 12 ambazo zimetawaliwa na Jua. Hivyo elimu hii inatumika Dunia nzima.
Kila mtu katika Dunia akitaka asitake, aamini au asiamini basi atakuwa amezaliwa katika moja wapo ya nyota hizi.
Basi mara nyingi mtu anapokuwa kazaliwa huwa anakuwa amechomozewa na moja kati ya MakundiNyota hizi 12.
Pia elewa ya kwamba nyota yako hiyo moja, unaweza ukakuta watu wanakwambia kwa tofauti tofauti pasipo kujua ipo katika kipengele gani, Kuna;
1: Nyota Iliyochomoza wakati unazaliwa. tunaita nyota ya kuzaliwa (Ascendant sign)
Nimeshaisema mara nyingi sana tangu 2014 mpaka leo bado naendelea kuwafundisha.
Pia kuna;
2: Nyota iliyochomoza tarehe na mwezi uliozaliwa yaani nyota ya jua (Sun sign/Zodiac Sign)
3: Nyota iliyochomoza wakati unazaliwa Mbalamwezi ilikuwa eneo gani. (Moon Sign)
4: Nyota iliyochomoza wakati unapewa jina lako. au nyota ya jina. (Name Sign)
Kuna moja ambayo ni ya ziada pia huwa tunaita letter sign yaani zile herufi za mtu za jina lake, Ama herufi za kwanza za mtu zinakuwa zinatoa jina gani. Lakini hizo ni dhaifu kwa maana zinakwenda kurudi kwenye Ascendant Signs (ambayo ni nyota iliyochomoza wakati mtu anazaliwa;
Lakini pia haiishii hapo inakwenda kugawanyika katika vipengele vya ziada 20 Hivyo tukiangalia mtawanyiko wa nyota yako tukiangalia wewe ni MakundiNyota fulani basi hapo tunakuwa hatujamaliza zaidi hicho kinakuwa ni kipengele kimoja kati ya vipengele 24.
Hii ndio sababu watu wengi wanapoangalia maswali ya nyota huona ni uzushi na uongo uliopindukia lakini wanashangaa na kuona wengine zinawang'aria na kupata mafanikio kinyota kwa kuifuata vyema, kufuatilia nyota si dhambi.
Hivyo basi; Ni elimu ya kusoma kama zilivyoelimu nyingine. Fahamu ya kwamba madaraja au mgawanyiko wa hizo sehemu za nyota yako ndio hutoa maelezo sahihi ya nyota yako.
Wengi wanawalipulia watu maelezo ya nyota vibaya na kuwafanya kupoteza kabisa ladha ya nyota zao na kuona nyota ni usanii fulani wa kubahatisha kipuuzi lakini ukweli sio hivyo.
Humo humo ndani ya nyota ndio kuna maelekezo ya wewe ni vipi unaweza kupata kitu fulani au tukio fulani kwa kufuata muongozo upi, na kufanya kipi.
Ili uweze kufanikisha jambo fulani basi angalia katika Chart yako nzima ya kuzaliwa ili uweze kuelewa sasa.
Na pia kwenye nyota hiyo utaweza kujua mambo unayotakiwa kuyafanya kila siku au kuyapangilia ili uweze kujua vipi unaweza kufuzu kinyota.
Nyota hizo zina athari kubwa katika maisha yako hasa ukitenda kinyume na matakwa ya nyota hiyo.
Mfano:
1: Ukifanya biashara ambayo siyo ya nyota yako, biashara hiyo itaathirika,
2: Uukimchukua mpenzi ambaye sio wa nyota yako bila kujua, mtapendana lakini mwisho utakuwa mbaya.
3: Ukifanya mambo ambayo nyota yako haikubaliani nayo mambo yako yatakwama na utajiona una mikosi.
Basi ninakuandalia video nyingi za nyota ili iweze kukusaidia kujitambua kuwasaidia, kufahamu undani kuhusu: nyota yako, mambo yanayohusu nyota hiyo, ikiwemo;
siku ya bahati, rangi,namba, nani wa kushirikiana nae kimapenzi, kikazi, kibiashara, jiwe gani uvae, manukato gani yanakufaa, mafusho ya nyota, mambo muhimu ya kufanya, Kipaji chako, mambo ya kujiepusha nayo, chakula chako, magonjwa yako, mpaka nchi za kukaa kama una uwezo au kujifananisha nao.
Ukifuatilia vizuri na kwa makini utaweza kujiepusha na matatizo mengi sana ya kimaisha, Ndoa zitadumu, biashara zitashamiri, na Mikosi itakuondokea.
Nyota zinatambulika kutokana na tarehe yako ya kuzaliwa,muda na saa au kama hujui basi inafaa na ndio bora zaidi kupigia hesabu jina lako la kuzaliwa pamoja na mama mzazi.
Sababu ya kutumia jina la mama mzazi kwa sababu yeye ndio ana uhakika zaidi ya kwamba wewe ni mtoto wake, na pia ana daraja kubwa kuliko baba katika uzani wa kiroho.
JINSI YA KUSOMA CHART YA UNAJIMU
• Jinsi ya kujua nyota | Jinsi ya kuangalia ...
JINSI YA KUJUA NYOTA YAKO
• Jinsi ya kuangalia Nyota? (Nyota yenye Pes...
NOTE:
Ikiwa unapendezwa,
╔═╦╗╔╦╗╔═╦═╦╦╦╦╗╔═╗
║╚╣║║║╚╣╚╣╔╣╔╣║╚╣═╣
╠╗║╚╝║║╠╗║╚╣║║║║║═╣
╚═╩══╩═╩═╩═╩╝╚╩═╩═╝
CONNECT WITH US!
========================================
FACEBOOK / / 61566429091668
INSTAGRAM / / rakimsspiritual
TIKTOK / / rakimsspiritual
X / https://x.com/rakimsspiritual/
WHATSAPP / https://api.whatsapp.com/message/VSDC...
========================================
Rakims Spiritual: https://www.Unajimu.com/
========================================
Rakims Spiritual.
Wasiliana nasi:
[email protected]
WhatsApp number
+255 783 930 601
Rakims Spiritual.
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: