🔴 RC RUVUMA AAGIZA KUSIMAMISHWA MKANDARASI ANAYETEKELEZA MRADI WA MILIONI 417 SONGEA DC
Автор: RUVUMA TV
Загружено: 2026-01-06
Просмотров: 162
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Brigedia Jenerali Ahmed Abasi Ahmed, ameagiza kusimamishwa kazi kwa mkandarasi wa Kampuni ya Bogeta Engineering Ltd anayesimamia mradi wa ujenzi wa madarasa, mabweni na vyoo katika Shule ya Sekondari Jenista Mhagama, iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Songea.
Akizungumza wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya elimu, RC Ahmed amesema mkandarasi huyo asimamishwe mara moja na kutafutwe mkandarasi mwingine atakayetekeleza mradi huo kwa kuzingatia masharti ya mkataba na kasi inayotakiwa na Serikali. Mradi huo unahusisha ujenzi wa mabweni mawili, madarasa sita na matundu kumi ya vyoo kwa gharama ya shilingi milioni 417.
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: