NI SIMANZI ISIYOFUTIKA MOYONI NDUGU WAKIKABIDHIWA MIILI 42 AJALI YA MABASI SAME
Автор: Mwananchi Digital
Загружено: 2025-07-03
Просмотров: 11505
Moshi. Ni siku iliyojaa huzuni, maumivu makali yasiyoelezeka, wakati familia 36 kati ya 42 zikiaga miili ya ndugu zao waliofariki ajalini Same, mkoani Kilimanjaro katika viwanja vya Hospitali Rufaa ya Kanda ya Kaskazini, KCMC.
Katika ajali hiyo zipo baadhi ya familia zimebaki bila baba, mama, babu, bibi, dada na kaka hali ambayo kwa binadamu wa kawaida ni ngumu kupokea kwa urahisi.
Ilikuwa ni siku ya Juni 28, mwaka huu ambayo ilikuwa ni siku ngumu kwa familia hizo kupokea taarifa ya ajali ya magari mawili kugongana uso kwa uso na kuteketea moto eneo la Sabasaba mjini Same, huku ndugu hao waliteketea kwa moto wakiwa ndani ya magari hayo.
Ajali hiyo ilitokea Juni 28, 2025 katika eneo la Sabasaba, Same mjini ikihusisha basi Kampuni ya Chanel One lililokuwa likitokea Moshi kwenda Tanga na basi dogo aina ya coaster lililokuwa likitokea Same mjini kwenda Moshi kugongana uso kwa uso na kuwaka moto wakati abiria wakiwa ndani ya magari hayo.
Waliofariki katika ajali hiyo ni watu 42, ambapo kwenye gari dogo aina Coaster walifariki watu 31 waliokuwa wanakwenda harusini mjini Moshi, huku kwenye basi la Chanel One wakifariki watu 11.
Akizungumza wakati miili hiyo ikiagwa leo mmoja wa wakilishi wa wafiwa, Kapteni Farijalla Mkojera amesema vifo vya ndugu zao ni msiba usiofutika mioyoni mwao na kwenye akili zao.
🎥 - Ombeni Daniel .
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: