IKUPA FINANCIAL SERVICE LTD YATOA AJIRA 200 KWA VIJANA
Автор: BONGO PLAY TELEVISION
Загружено: 2026-01-19
Просмотров: 28
Kampuni isiyo ya serikali ya Kutoa Mikopo kwa Wajasiliamali, Ikupa Financial Service Ltd, imetoa ajira kwa vijana wapatao 200 katika maeneo mbalimbali nchini
Akizungumza mkurugenzi wa kampuni hiyo Ikupa Mwaifwani katika sherehe maalumu iliyowakutanisha wafanyakazi na wateja wa kampuni hiyo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 12 tangu kuanzishwa kwake. Katika hafla hiyo, ambapo ameeleza fahari yake kwa mafanikio yaliyopatikana, ikiwemo kutoa ajira kwa zaidi ya vijana 200 pamoja na kuwawezesha Watanzania wengi kupata mikopo iliyowasaidia kuanzisha, kukuza na kuendeleza biashara zao sambamba na ukuaji wa kampuni.
Aidha, Mkurugenzi huyo amesema Ikupa Financial Service Ltd imeendelea kuwa mstari wa mbele kuwaunga mkono wakulima kwa kuwapatia mikopo kulingana na mahitaji yao kwa kipindi cha miezi sita, ambapo marejesho hufanyika baada ya mavuno. Kwa upande wao, wanufaika wa mikopo hiyo wameeleza kuridhishwa na huduma zinazotolewa, wakibainisha kuwa mikopo imeongeza uzalishaji, kuimarisha shughuli zao za kiuchumi na kuwajengea imani ya kuendelea kushirikiana na taasisi hiyo kwa maendeleo endelevu.
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: