Namna ya kumsaidia mtoto kupumua wakati wa kuzaliwa
Автор: BMG ONLINE TV
Загружено: 2017-11-16
Просмотров: 813
Ni katika ukumbi wa Nyakahoja Jijini Mwanza ambapo Wakunga na Madaktari wa kutoka Zahanati, Vituo vya Afya pamoja na Hospitali za binafsi Kanda ya Ziwa, wanakutana kwa ajili ya kupata mafunzo ya kuwasaidia watoto wanaopata matatizo ya kupumua wakati wa kuzaliwa.
Lengo ni kuhakikisha hakuna kifo cha mtoto kinachotokana na matatizo ya kupumua wakati wa kuzaliwa ikizingatiwa kwamba takribani asilimia 10 ya watoto wanaozaliwa hupata matatizo ya kupumua wakati wa zoezi hilo.
Mafunzo hayo yamefadhiliwa na Chama cha Watoa Huduma za Afya Tanzania APHFTA kwa kushirikiana na Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho.
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: