ROZARI SARA MUHIMU SANA -ROZARI SIO HIRIZI.
Автор: Mawaridi Media
Загружено: 2024-10-24
Просмотров: 114
*ROZARI - SALA MUHIMU SANA.
ROZARI SIO HIRIZI
Kuna wapinzani wa Imani yetu wanaodai kuwa, Eti, Rozari ni Hirizi.
HATUKATAI ukweli kwamba;
Kuna uwezekano wa mtu KUITUMIA rozari VIBAYA kama vile mtu anavyoweza kumwabudu mchungaji fulani, aina ya ibada (matambiko), tumafuta twa upako, na kadhalika.
Lakini rozari yenyewe si aina ya ibada ya sanamu
Kama tulivyoona tangu awali, Rozari ni chombo maalum tunachokitumia kutuongoza katika Tafakari ya Sala.
Rozari inatusaidia sana Kwani, Sala yoyote inaweza kupoteza maana yake ikiwa hatusali tukitafakari kimakusudi.
Lakini
Kunaweza kukawa na watu wanaoitumia Rozari kwa malengo mengine tofauti na Sala.
Kwamfano, kuna watu WANAOCHIMBIA Rozari katika maeneo ya nyumba zao sawa na wale wanaochimbia mahirizi kulinda nyumba zao.
Watu wengine wametundika Rozari kila mahali iwe ni kwenye magari yao, milangoni mwa nyumba, vitandani mwao na maofisini kama Kinga na Ulinzi.
Kuna wanaovaa Rozari SEHEMU mbalimbali za mwili kama vile kiunoni, mikononi na hata miguuni kama KINGA mithili ya Mahirizi.
Yote hayo tunaweza kusema ni MATUMIZI MABAYA ya Rozari tofauti na lengo hasa lililo kusudiwa la Sala.
Lakini;
Kuna watu wengi wenye mazoea ya kuvaa Rozari shingoni au kuziweka mifukoni.
Kufanya hivyo sio vibaya ikiwa kama nia yake ni kuzingatia Sala.
Ni jambo jema kuweka rozari yako karibu kama ukumbusho wa Kusali au
Kuiweka karibu na kuwa tayari kuitumia wakati wowote unapohitaji kuitumia katika Sala.
Lakini, Sala ya Rozari ni chombo madhubuti cha kumlinda Mtu.
Sio Punje za Rozari zilizo na uwezo wa kumlinda Mtu bali Sala ya Rozari inayosaliwa kwa Tafakari kutumia chombo Kitakatifu kiitwacho Rozari.
Tunasema Rozari ni chombo Kitakatifu kwasababu, kimewekwa wakfu au KIMETENGWA kwa ajili ya Mungu.
Sala ya Rozari imethibitika kuwa na nguvu ya kimiujiza ya kuwalinda wale wa imani na kuwapa neema za ziada.
Kwamfano Sala ya Rozari inajulikana kusaidia ushindi katika vita vya zamani vya Wakristo dhidi ya Majeshi ya maadui zao.
Watakatifu wengi wakuu katika historia, wakiwemo Papa Yohane Pauli II, Padre Pio, na Lucia wa Fatima, walitambua Sala ya Rozari kama silaha yenye nguvu zaidi katika kupigana vita vya kweli vya kiroho tunavyokabiliana navyo duniani.
Maandiko Matakatifu yanasema;
Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama, bali ni juu ya falme na mamlaka, na wakuu wa giza hili la sasa, pamoja na pepo wabaya katika mbingu” (Waefeso 6:11–12).
Paulo anasisitiza kusema;
Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani (Waefeso 6:11).
Mojawapo ya Silaha hizi ni SALA.
Sala ya Rozari ni silaha yenye nguvu ya kuwakimbiza mapepo na kujiweka mbali na dhambi…
Ikiwa kama tunataka amani mioyoni mwetu, katika nyumba zetu, na katika nchi yenu, basi tujitahidi Kusali Sala ya Rozari. Isipite hata siku moja bila Kusali Rozari, haijalishi umeelemewa kiasi gani na masumbuko na kazi nyingi.
Mtu anaweza kuhoji; Je huko sio kumtukuza Bikira Maria?
Jibu ni HAPANA kwasababu, Rozari si sala kwa Bikira Maria.
Tumsifu Yesu Kristo
#mawaridimedia
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: