MHITIMU WA DARASA LA SABA ALIVYOGEUZA UWANJA WAKE KUWA KITUO CHA MALEZI YA WATOTO
Автор: Makutano TV
Загружено: 2025-07-23
Просмотров: 241
IRINGA (Ipogolo C)Kwa mujibu wa takwimu za Serikali, hadi kufikia mwaka huu, 2025, ni vituo 206 pekee vya kulele watoto mchana, vitakuwa vimeanzishwa nchi nzima kwa watoto wa umri wa Miaka 2 hadi 5.
Pia Takwimu za sensa ya mwaka 2022 zinaonyesha zaidi ya watoto milioni 9 wana umri wa Miaka 0 hadi 5 hapa Nchini Tanzania.
Watoto hawa wote, Kila mmoja anastahili mwanzo bora. swali ni Je? hapo ulipo watoto wana mwanzo bora?
Vituo vya kulelea watoto mchana ni nyenzo muhimu ya mtoto kuwa na mwanzo bora wa maisha yake, Hapa ni Kata ya Ruaha Manispaa ya Iringa mtaa wa Ipogolo C.
Mtaa wa Ipogolo C ni miongoni mwa mitaa 13 iliyopo katika kata hii, yenye jumla ya Kaya zaidi ya elfu 3 na 500, katikati ya makazi ya watu ndipo tunakutana na Ndugu Matuli Kavela.
Elimu yake ni darasa la saba, kutokana uchumi duni hakuweza kuendelea na elimu ya sekondari, ana Miaka 50, baba mwenye watoto 5 na wajukuu wanne, hapa ni nyumbani kwake ambapo sasa anatoa huduma ya malezi jamii mchana.
Kutoka watoto 3 hadi kufikia watoto 70 kwa Miaka hii mitatu, sio jambo rahisi, Matuli anasema Imani ya wazazi kwake ndio msukumo wake kutoa huduma hiyo ya malezi ya watoto mchana
Licha ya ulemavu wake, Changamoto ya mazingira duni, uhaba wa vifaa vya kufundishia na kutokuwa na ujuzi wa malezi sio kikwazo kwake kuhudumia watoto hawa, anasema kikwazo ni agizo alilolipata la kumtaka asitishe huduma hiyo jambo ambalo limemvunja moyo.
Ushiriki wa wazazi, jamii, Serikali, na wadau ni msingi wa kuhakikisha watoto hawa wanapata mazingira salama yenye upendo na yenye kuhamasisha ukuaji mzuri wa akili, mwili na hisia ili kuweka msingi thabiti wa maisha yao Wananchi na wazazi wao wanasemaje?
UNGANA NASI KATIKA MAKALA INAYOFUATA UWEZE KUSIKIA KAULI YA SERIKALI NA WADAU HASA WAKATI HUU AMBAPO SERIKALI INATEKELEZA KAMPENI YA MALEZI, NA PROGRAMU JUMUISHI YA MALEZI MAKUZI NA MAENDELEO YA AWALI YA MTOTO
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: