KOROSHO MARATHON KUENDELEA KUTANGAZA FURSA ZA UWEKEZAJI KATIKA TASNIA YA KOROSHO
Автор: Cashewnut Boardtz
Загружено: 2025-11-29
Просмотров: 25
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Maendeleo ya Vijana, Mhe. Joel Nanauka, amesema kuwa mbio za Korosho Marathon zimekuwa jukwaa muhimu la kutangaza fursa za uwekezaji katika tasnia ya korosho, kuhamasisha afya kwa kufanya mazoezi, pamoja na kuelimisha jamii juu ya ulaji wa korosho na matumizi ya bidhaa mbalimbali zitokanazo na zao hilo.
Ametoa kauli hiyo katika viwanja vya Millenium, mkoani Mtwara, wakati wa mbio za Korosho Marathon zilizofanyika Novemba 29, 2025. Aidha, amesema kuwa lengo mahususi la mbio hizo ni kupanua wigo wa soko la ndani la korosho ili kuchochea ukuaji wa uchumi wa mtu mmoja mmoja na wa Taifa kwa ujumla.
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: