U Mwendo Gani Nyumbani | Irene Michael | Nyimbo Za Kristo
Автор: Nyimbo Za Kristo SDA
Загружено: 2025-07-13
Просмотров: 17895
Mpendwa mtazamaji karibu.. na ubarikiwe na nyimbo katika channel yetu
Singer: Irene Michael
Song: U mwendo Gani Nyumbani
Producer: Mr RJ | RJ STUDIO
You are welcome
Lyrics
U mwendo gani nyumbani? Mlinzi akanijibu,
"Usiku sasa waisha, macheo karibu."
Usihuzunike tena, bali ulemee mwendo
Hata ushike ufalme kule mwangani juu.
Na tena niliuliza, nchi yote ikajibu:
"Sasa mwendo watimika, milele karibu."
Usihuzunike tena, ishara kuu zasonga
Na viumbe vyangojea sauti ya Bwana.
Nikamwuliza shujaa, ndivyo kanitia moyo:
"Shikilia mapigano, kitambo yaisha."
Usihuzunike tena, kazi ifanywe kwa moyo;
Tumeahidiwa tunu tuishapo shinda.
Siyo mbali na nyumbani! fikara tamu njiani,
Latupoza roho, nalo lafuta machozi.
Usihuzunike tena, kitambo tutakutana
Wenye furaha kamili nyumbani mwa Baba.
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: