Популярное

Музыка Кино и Анимация Автомобили Животные Спорт Путешествия Игры Юмор

Интересные видео

2025 Сериалы Трейлеры Новости Как сделать Видеоуроки Diy своими руками

Топ запросов

смотреть а4 schoolboy runaway турецкий сериал смотреть мультфильмы эдисон
dTub
Скачать

RAIS MWINYI ASISITIZA UMUHIMU WA AMANI KWA MAENDELEO YA TAIFA

Автор: MAISHA ONLINETV

Загружено: 2025-11-28

Просмотров: 1125

Описание:

RAIS MWINYI ASISITIZA UMUHIMU WA AMANI KWA MAENDELEO YA TAIFA

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema kuwa kuna umuhimu mkubwa kwa kila Mwananchi kutimiza wajibu wake katika kudumisha Amani.

Rais Dkt. Mwinyi ametoa wito kwa makundi ya Wanasiasa, Viongozi wa Dini na Waandishi wa Habari kuwa makini na kauli wanazozitoa mbele ya jamii kwa kuwa ndio makundi yanayosikilizwa na watu wengi na yenye ushawishi mkubwa katika jamii.

Alhaj Dkt. Mwinyi ameyasema hayo leo tarehe 28 Novemba 2025 alipojumuika na Waumini wa Dini ya Kiislamu katika Sala ya Ijumaa na Dua Maalumu ya Kumshukuru Mungu pamoja na kuiombea Taifa Amani.

Dua hiyo imesomwa katika Msikiti wa Jamiu Zinjibar, Kiembe Samaki, Mkoa wa Mjini Magharibi.

Amefafanua kuwa matukio yaliyojitokeza Tanzania Bara ni funzo muhimu kwa Watanzania wote, ikiwemo Zanzibar, kwamba hakuna jambo linaloweza kufanikiwa bila kuwepo kwa Amani katika nchi.

Ameeleza kuwa si suala la maendeleo pekee bali hata ibada haziwezi kufanyika panapokosekana Amani.

Amewasisitiza Wanasiasa, Viongozi wa Dini na Waandishi wa Habari kuendelea kuhubiri na kuimarisha Amani wakati wote.

Rais Dkt. Mwinyi amewataka Viongozi wa Dini zote kuwa na kauli zinazohimiza Amani kwa wafuasi wao, na kuwataka Waandishi wa Habari kutumia kalamu zao na mitandao ya kijamii kwa busara, na kuacha kuchapisha habari zinazoathiri Amani ya nchi.

Aidha, Rais Dkt. Mwinyi ameishukuru Afisi ya Mufti kwa kuandaa Dua hiyo maalum ya kuiombea nchi Amani na kumshukuru Mungu kwa kuijalia Nchi utulivu kabla, wakati na baada ya Uchaguzi.

Akitoa salamu za Afisi ya Mufti, Katibu Mtendaji Sheikh Khalid Ali Mfaume amewahimiza Wananchi wa Tanzania, ikiwemo Zanzibar, kuithamini na kuipenda Nchi yao kwa kuwa ndio Taifa walilobarikiwa na Mwenyezi Mungu.

Amesisitiza kuwa kila mmoja, hususan Vijana, wanapaswa kulithamini Taifa lao na kuishi maisha yenye Nidhamu na Hekima kila siku.

RAIS MWINYI ASISITIZA UMUHIMU WA AMANI KWA MAENDELEO YA TAIFA

Поделиться в:

Доступные форматы для скачивания:

Скачать видео mp4

  • Информация по загрузке:

Скачать аудио mp3

Похожие видео

Mambo yanayofanyika hudhani waliojipa madaraka ni Waislamu | GUMZO LA LEO

Mambo yanayofanyika hudhani waliojipa madaraka ni Waislamu | GUMZO LA LEO

RAIS MWINYI KATIKA DUA YA KUIOMBEA NCHI PEMBA

RAIS MWINYI KATIKA DUA YA KUIOMBEA NCHI PEMBA

Why Tanzanians Say ‘Zanzibar Ni Nchi Ndani Ya Nchi’ — Kero za Muungano 🇹🇿

Why Tanzanians Say ‘Zanzibar Ni Nchi Ndani Ya Nchi’ — Kero za Muungano 🇹🇿

"UJUMBE MZITO" SHEKH WALID AVUNJA UKIMYA ATOA KAULI NZITO ILIYOWAPONYA WAUMINI WA KICHANGANI NA UMMA

Historia ya Mzee Mwinyi, asili yake, familia yake, siasa na urais mara mbili Bara na Zanzibar

Historia ya Mzee Mwinyi, asili yake, familia yake, siasa na urais mara mbili Bara na Zanzibar

HABARI KUBWA KUTOKA TANZANIA ASUBUI HII..

HABARI KUBWA KUTOKA TANZANIA ASUBUI HII..

Baada ya kusema wanafunzi na wazazi Z'bar waache udanganyifu kwenye mitihani wadau wamjia juu Zena

Baada ya kusema wanafunzi na wazazi Z'bar waache udanganyifu kwenye mitihani wadau wamjia juu Zena

EXCLUSIVE: AMANI KARUME ATEMA CHECHE, AFUNGUKA SAKATA LA BANDARI

EXCLUSIVE: AMANI KARUME ATEMA CHECHE, AFUNGUKA SAKATA LA BANDARI

KUMEKUCHA SIASA ZA ZANZIBAR / Dkt. MWINYI KUMUACHIA KITI OTHAMAN MASOUD?/ ATAJWA NI MTU WA AINA GANI

KUMEKUCHA SIASA ZA ZANZIBAR / Dkt. MWINYI KUMUACHIA KITI OTHAMAN MASOUD?/ ATAJWA NI MTU WA AINA GANI

BILA YA KITAMBULISHO MARUFUKU KUINGIA ZANZIBAR

BILA YA KITAMBULISHO MARUFUKU KUINGIA ZANZIBAR

Mwisho wa Kiburi ni Maangamizi | TAHARIRI YA GUMZO

Mwisho wa Kiburi ni Maangamizi | TAHARIRI YA GUMZO

1,3 ТРИЛЛИОНА РУЗУКУ ПОЛУЧАЕТ КАТОЛИЧЕСКАЯ ЦЕРКВЬ, МУСУЛЬМАНЕ НЕ ПОЛУЧАЮТ НИЧЕГО — ШЕЙХ САИД КИНЁ...

1,3 ТРИЛЛИОНА РУЗУКУ ПОЛУЧАЕТ КАТОЛИЧЕСКАЯ ЦЕРКВЬ, МУСУЛЬМАНЕ НЕ ПОЛУЧАЮТ НИЧЕГО — ШЕЙХ САИД КИНЁ...

Tuwaeleze ukweli Viongozi wetu wanapokosea, tusijikweze.

Tuwaeleze ukweli Viongozi wetu wanapokosea, tusijikweze.

Արմեն Չիբուխչյան - Վերլուծություններ ARTN լրատվականում 12-08-25

Արմեն Չիբուխչյան - Վերլուծություններ ARTN լրատվականում 12-08-25

RAIS SAMIA AWALIPUA MAASKOF WA TEC, HAMNA MAMLAKA ,NCHI INAONGOZWA KIKATIBA MATAMKO 8 MMENITOLEA

RAIS SAMIA AWALIPUA MAASKOF WA TEC, HAMNA MAMLAKA ,NCHI INAONGOZWA KIKATIBA MATAMKO 8 MMENITOLEA

WAANGALIE WATUMBATU, WAPEMBA NA WAMAKUNDUCHI WAKIIGIZA PAMOJA.

WAANGALIE WATUMBATU, WAPEMBA NA WAMAKUNDUCHI WAKIIGIZA PAMOJA.

HAYA HAPA MANENO MAZITO ALIYO YASEMA MBETO MBELE YA VIJANA  MKOA WA KUSINI PEMBA

HAYA HAPA MANENO MAZITO ALIYO YASEMA MBETO MBELE YA VIJANA MKOA WA KUSINI PEMBA

OTHMAN MASOUD AWEKA WAZI KUCHUKUA HATUA AMBAZO ZINA WABABAISHA CCM ZANZIBAR

OTHMAN MASOUD AWEKA WAZI KUCHUKUA HATUA AMBAZO ZINA WABABAISHA CCM ZANZIBAR

OTHMAN MASOUD KWA AZUNGUMZA MANENO HAYA KWA UCHUNGU TUSIKUBALI TUKAPOTEZWA

OTHMAN MASOUD KWA AZUNGUMZA MANENO HAYA KWA UCHUNGU TUSIKUBALI TUKAPOTEZWA

#WAZIRI HAMZA AMTOLEA UVIVU MANGI KIMAMBI

#WAZIRI HAMZA AMTOLEA UVIVU MANGI KIMAMBI

© 2025 dtub. Все права защищены.

  • Контакты
  • О нас
  • Политика конфиденциальности

Контакты для правообладателей: [email protected]