KIJITONYAMA LUTHERAN CHURCH : IBADA YA EVENING GLORY - THE SCHOOL OF HEALING 11 DECEMBER 2025
Автор: KIJITONYAMA LUTHERAN CHURCH
Загружено: 2025-12-12
Просмотров: 3261
KIJITONYAMA LUTHERAN CHURCH : IBADA YA EVENING GLORY - THE SCHOOL OF HEALING 11 DECEMBER 2025
SIKU YA 39 YA MAFUNGO YA KUMALIZA MWAKA 2025 NA KUOMBEA MWAKA 2026
MADA: "FROM HOW TO WHO" (INAWEZEKANA)
NENO KUU: "HOW SHALL THIS BE?" (LITAKUWAJE NENO HILI?)
UJUMBE WA LEO: KUZUILIWA KUWA
[MIKAKATI YA KIROHO]
Kutoka 3 : 19
Daniel 9 : 22
Zaburi 50:5
Wakolosai 1 : 13
Mwanzo 26 : 1 - 5, 12
MKAKATI WA KIMAJIRA NA WATU SAHIHI
MKAKATI WA KIAGANO
[Maisha ya Kiagano]
AGANO LA KURITHI
3. UBORA au UBAYA wa kinachopatika kwenye AGANO ambalo mtu amerithi kinategemea ni Mungu yupi aliyehusishwa kwenye hilo AGANO.
Kumbuka:
A. AGANO linampa mtu/watu Aina ya Maisha wanayopaswa Kuishi
( Ubora wa Maisha unategemea UBORA wa Mungu aliyehusishwa kwenye hilo AGANO )
B. Kama kuna AGANO mtu amerithi hata kama halijui wala Mungu aliyehusishwa Hamjui hakuzuii :
Kutokuguswa na kilichopo kwenye AGANO
Mungu aliyehusishwa kwenye AGANO kufuatilia Maisha yake
Kuadhibiwa kama akienda Tofauti na Masharti ya AGANO.
4. Mungu aliyehusishwa Kwenye AGANO atafuatilia Mengi katika Uzao vizazi na vizazi Mfano:
A. Watu wa Kuambatana nao na wabebe nini kwa ajili yako
( Wakufae wapi? )
B. Eneo la NDOA (Kuoa na Kuolewa)
C. Mahusiano yao Binafsi na Huyo Mungu.
D. Eneo la UCHUMI.
Wanapopata MSAADA wa Kiroho
Namna ya Matumizi ya Mafanikio yao.
Kutoka 3 : 19
19 Nami najua ya kuwa huyo mfalme wa Misri hatawapa ruhusa mwende zenu, la, hata kwa mkono wa nguvu.
Daniel 9 : 22
22 Akaniagiza, akaongea nami, akasema, Ee Danieli, nimetokea sasa, ili nikupe akili upate kufahamu.
Zaburi 50 : 5
5 Nikusanyieni wacha Mungu wangu Waliofanya agano nami kwa dhabihu.
Wakolosai 1 : 13
13 Naye alituokoa katika nguvu za giza, akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme wa Mwana wa pendo lake;
Mwanzo 26 : 1 - 5, 12
1 Ikawa njaa katika nchi hiyo, mbali na njaa ile ya kwanza iliyokuwa siku za Ibrahimu. Isaka akamwendea Abimeleki, mfalme wa Wafilisti, huko Gerari.
2 Bwana akamtokea, akasema, Usishuke kwenda Misri, kaa katika nchi nitakayokuambia.
3 Kaa ugenini katika nchi hiyo, nami nitakuwa pamoja nawe, na kukubariki, maana nitakupa wewe na uzao wako nchi hizi zote. Nami nitakifanya imara kiapo nilichomwapia Ibrahimu baba yako.
4 Nitazidisha uzao wako kama nyota za mbinguni, nami nitawapa uzao wako nchi hizi zote, na katika uzao wako mataifa yote ya dunia watajibarikia.
5 Kwa sababu Ibrahimu alisikia sauti yangu, akayahifadhi maagizo yangu, na amri zangu, na hukumu zangu, na sheria zangu.
12 Isaka akapanda mbegu katika nchi ile, akapata mwaka ule vipimo mia kwa kimoja, Bwana akambariki.
Mwanzo 26 : 24
24 Bwana akamtokea usiku uleule, akasema, Mimi ni Mungu wa Ibrahimu baba yako, usiogope, maana mimi ni pamoja nawe, nami nitakubarikia, na kuzidisha uzao wako kwa ajili ya Ibrahimu mtumishi wangu.
Mwanzo 28 : 13
13 Na tazama, Bwana amesimama juu yake, akasema, Mimi ni Bwana, Mungu wa Ibrahimu baba yako, na Mungu wa Isaka; nchi hii uilalayo nitakupa wewe na uzao wako.
Kutoka 2 : 23 - 25
23 Hata baada ya siku zile nyingi mfalme wa Misri akafa; wana wa Israeli wakaugua kwa sababu ya ule utumwa, wakalia; kilio chao kikafika juu kwa Mungu kwa sababu ya ule utumwa.
24 Mungu akasikia kuugua kwao, Mungu akakumbuka agano lake alilolifanya na Ibrahimu na Isaka na Yakobo.
25 Mungu akawaona wana wa Israeli, na Mungu akawaangalia.
2 Wafalme 17 : 25 - 26
25 Basi ikawa, wakati ule walipoanza kukaa huko, hawakumcha Bwana; kwa hiyo Bwana akapeleka simba kati yao, nao wakawaua baadhi yao.
26 Kwa hiyo wakamwambia mfalme wa Ashuru, wakasema, Wale wa mataifa uliowahamisha, na kuwaweka katika miji ya Samaria, hawaijui kawaida ya Mungu wa nchi; kwa hiyo amepeleka simba kati yao, na tazama, wanawaua, kwa sababu hawaijui kawaida ya Mungu wa nchi.
Isaya 43 : 4
4 Kwa kuwa ulikuwa wa thamani machoni pangu, na mwenye kuheshimiwa, nami nimekupenda; kwa sababu hiyo nitatoa watu kwa ajili yako; na kabila za watu kwa ajili ya maisha yako.
Kutoka 34 : 15 - 16
15 Usije ukafanya agano na wenyeji wa nchi, watu wakaenda kufanya uzinzi na miungu yao, na kuitolea sadaka miungu yao; mtu mmoja akakuita, ukaila sadaka yake.
16 Ukawaoza wana wako binti zao, nao binti zao wakaenda kufanya uzinzi na miungu yao, wakawavuta wana wenu wafanye uzinzi na miungu yao.
Yoshua 24 : 15
15 Nanyi kama mkiona ni vibaya kumtumikia Bwana, chagueni hivi leo mtakayemtumikia; kwamba ni miungu ile ambayo baba zenu waliitumikia ng'ambo ya Mto, au kwamba ni miungu ya wale Waamori ambao mnakaa katika nchi yao; lakini mimi na nyumba yangu tutamtumikia Bwana.
Mhubiri: Mwl.Eng. Goodluck Mushi
Kwa maombi na ushauri :
Mch. Kiongozi: Dr. Eliona Kimaro
Simu: +255 655 516 053, +255 754 516 053
Mch. Msaidizi: Anna Kuyonga
Simu: +255 713 553 443
YouTube: Kijitonyama Lutheran church
Barua Pepe : [email protected]
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: