Wimbo wa Tafakari wa Wiki | Huruma ya Mungu kwa Waliopoteza Maisha | Sala ya Amani kwa Taifa
Автор: MLANGO WA IMANI MEDIA
Загружено: 2025-11-15
Просмотров: 168
Katika video hii ya “Wimbo wa Tafakari wa Wiki,” tunatafakari juu ya Huruma ya Mungu Wetu kwa wale wote waliopoteza maisha kwa kupigwa risasi wakati wa uchaguzi.
Ni tafakari ya majonzi, sala, na matumaini — tukimwomba Mungu azipokee roho za marehemu katika nuru ya milele na azipe faraja familia zote zilizoguswa.
Tunaliombea pia taifa letu:
✨ Mungu atuletee amani
✨ Atuongoze katika haki
✨ Atuepushe na umwagaji damu
✨ Aweke mkono wake juu ya watu wake
Ee Bwana wa huruma, wapokee watoto wako katika amani ya milele, uwaponye waliojeruhiwa moyoni, na ulinde taifa letu katika upendo na umoja.
Amani iwe juu ya Tanzania.
Requiescat in pace.
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: