JGM KATIKA MAADHIMISHO YA MIAKA 60 KANISA KUU MOROGORO
Автор: Rev.Can.Wilson Mafumbi
Загружено: 2025-11-30
Просмотров: 174
Kwaya ya JGM Kanisa Anglikana Tanzania
Dayosisi ya Morogoro
HISTORIA FUPI KANISA KUU LA UTATU MTAKATIFU MOROGORO
Kanisa Kuu la Utatu Mtakatifu Morogoro ndilo Kanisa Kuu la Dayosisi ya Morogoro. Kanisa hili lilijengwa na Wamisionari miaka ya 1920, wakati likiwa chini ya Dayosisi ya Central Tanganyika. Jengo jipya la Kanisa la Utatu Mtakatifu lilifunguliwa tarehe 7 Agosti mwaka 1960 na Askofu wa Dayosisi ya Central Tanganyika Baba Askofu Alfred Stanway.
Kanisa lilipanuliwa na kuliongeza upana pande zote mbili kuanzia mwaka 1992 wakati wa Askofu Dudley Mageni. Upanuzi huo ulifanya kaburi la Askofu Yohana Omari kuwa ndani ya kanisa, hapo awali lilikuwa nje ya kanisa upande wa kushoto unapoingia kanisani.
Sinodi ya kwanza ya Dayosisi iliyofanyika tarehe 1 Desemba 1965 siku ya Jumatano,Sinodi hii ilifanyika Shule ya Biblia Morogoro katika Kanisa la Emmanueli iliamuakuwa Kanisa la Utatu Mtakatifu Morogoro kuwa Kanisa Kuu (Cathedral)
Akiandika katika Gazeti la Upanga wa Roho toleo la Oktoba 1960 Pasta wa Mtaa wa Morogoro wakati huo Kasisi Richard Kadege alisimulia hivi:
Rev. Canon Richard . A. Kadege
Mnamo tarehe 7 ya Mwezi wa Agosti tulikuwa na furaha ya ajabu sana ya kufurahia sikukuu ya kufunguliwa kwa kanisa letu jipya, linaloitwa “Utatu Mtakatifu” (Holy Trinity).
Kuanzia siku ya Jumamosi wageni mbalimbali walianza kufika. Pia wageni maarufu wa mji walialikwa wengi kati ya hao wageni wengine pia ambao ni maarufu walikuwapo Maaskofu ambao walikuwa wanne, kwanza Askofu wa Uaskofu huu Alfred Stanway na Yohana. M. Omari Askofu wa Ukaguru na Unguu, F. H. Olang’ Askofu wa Maseno, Kenya, na Askofu Mhindi aliyetoka Bara Hindi ya Kusini ambaye ni wa Kanisa la Mar Thoma.
Zilifika Kwaya tatu, ya kwanza ilitoka Ibwaga Kongwa, ya pili Zoisa, ya tatu Ukagulu. Hivyo Kanisa lilijaa wageni ambao idadi yao inafika kama mia tano na wenyeji ambao walikaa nje walikaribia mia tatu. Hivyo Kwaya ziliimba nyimbo zao ambazo zilikuwa za Neno la Mungu.
Ibada ilianza saa tatu na nusu asubuhi na Baba Mheshimiwa katika Mungu baada ya kuombwa na wazee afungue Kanisa alikubali kufanya hivyo, Askofu wa Uaskofu huu Alfred Stanway alianza kwa kugonga mlango, yaani kupiga hodi na fimbo yake ndipo wazee walimfungulia mlango. Yeye na Maaskofu wengine na Makasisi wakaingia, jumla ya Makasisi waliohudhuria ni kumi na sita pamoja na Maachideacon watatu.
Hapo Askofu Alfred Stanway alianza kubariki kila mahali mle Kanisani ambapo Ibada ya Mungu itakuwa ikifanywa, na baada ya kubariki ndipo Kwaya ya Zoiza iliimba wimbo wa kumkaribisha Askofu kwa mahubiri yake na neno lake lilikuwa Luka 19:46b. Lisemalo “Nyumba yangu itakuwa nyumba ya Sala,” hivyo Bwana akatufunulia mengi katika maisha yetu na jinsi tulivyoweza kuitimiza nyumba yake na kuiheshimu.
Askofu Alfred Stanway aliendelea kwa Kiingereza na Askofu R. Olang’ akatafsiri kwa Kiswahili, na tuliweza kupokea Baraka za ajabu, shukrani kwa wote ambao walichukua mzigo wa kuiombea siku ile Mungu azidi kusema na watu wake katika nyumba yake.
R. A. Kadege
Pastor wa Mtaa wa Morogoro
Tangu kuanzishwa kwa Dayosisi ya Morogoro, Kanisa hili limekuwa ndilo Kanisa Kuu la Dayosisi. Tarehe 30 Novemba 1965 Dayosisi ya Morogoro ilipoanzishwa rasmi; Kanisa Kuu la Utatu Mtakatifu limekuwa chini ya Uongozi wa Baba Maaskofu wafuatao (Dean wa Kanisa Kuu) Baba Askofu Gresford Chitemo 1965 – 1987, Baba Askofu Dudley Mageni 1987 – 2008, na Baba Askofu Godfrey Sehaba kuanzia 2008….
Makasisi Viongozi waliohudumu Kanisa Kuu la Utatu Mtakatifu kuanzia mwaka 1965 ni: Kasisi Sifael Maulidi, Kasisi Canon Richard Kadege, Kasisi Lesilei Chidoge 1970 – 1975, Kasisi Canon Charles Almodad Munga 1976 – 1979, Kasisi Kenedy Kisanga 1980 – 1981, Kasisi Canon Isaka Msegu 1982 – 1988, Kasisi Canon Yeremia Malekela 1989 – 1991, Kasisi Canon Fanuel Makau 1991 – 1994, na Kasisi Canon Yeremia Malekela 1995 – 1998. Wengine ni Kasisi Canon Lupyana Mgimba 1998
– 2006, Kasisi Canon Stephano Machila 2006 – 2008, Kasisi Canon Charles Almodad Munga 2008 – 2010, Kasisi Canon James Mligite 2010 – 2013, na Kasisi Frederick Stephen Chingwaba 2013, Kasisi Canon Peter Mkengi mpaka Sasa. Kanisa Kuu la Utatu Mtakatifu lipo Morogoro Mjini.
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: