MSIMU WA TOHARA WASOGEZWA MBELE KUPISHA UCHAGUZI
Автор: Afri Pic
Загружено: 2025-10-17
Просмотров: 313
Laigwanan Mkuu wa Jamii ya Kimasai nchini Tanzania Bwana Isack Ole Kisongo Meijo ametangaza kusogezwa mbele kwa zoezi la tohara kwa Vijana wa kimasai lililokuwa lifanyike kuanzia Oktoba 21-30 mwaka huu ili kutoa fursa kwa Vijana zaidi ya 2,000 waliokuwa washiriki kwenye zoezi hilo kwenda kupiga kura kwenye uchaguzi Mkuu Oktoba 29, 2025.
Ole Kisongo ametoa maelezo hayo leo oktoba 17, 2025 mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. CPA Amos Gabriel Makalla wakati wa Baraza la Maigwanani Mkoa wa Arusha, akimuhakikishia Mkuu wa Mkoa kuwa wapo tayari kwa uchaguzi na kulinda kulinda amani wakati wote wa uchaguzi Mkuu kwenye jamii yao.
"Hiyo siku ni takatifu katika Taifa la Tanzania, Hiyo siku ni njema na tumeambiana jamii ya kimasai kuwa hatujawahi kushika mkia, tunataka kujitokeza kwa wingi kupiga kura katika Vijiji vyetu sasa Ukitahiri Vijana 1,000 leo utapunguza kura kwani Mgonjwa atashindwa kwenda kupiga kura. Tunataka kushiriki vyema kupiga kura sote." Amesisitiza Ole Kisongo.
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: