DC SITTA AONDOA MGOGORO WA MIAKA 10 KATI YA HALMASHAURI YA IRINGA NA VIJIJI VIWILI KILOLO
Автор: PAMLOMO24
Загружено: 2025-11-25
Просмотров: 41
Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Benjamin Sitta, amefanikiwa kusuluhisha mgogoro uliodumu kwa zaidi ya miaka 10 kati ya Halmashauri ya Wilaya ya Iringa na serikali za vijiji vya Bomalang’ombe na Lyamko wilayani Kilolo. Mgogoro huo ulikuwa ukihusisha umiliki na usimamizi wa hisa za kampuni ya Bomalang’ombe Village Company Limited (BVC), inayotekeleza miradi mbalimbali ikiwemo uzalishaji wa umeme na usindikaji wa matunda.
Hayo yamebainika leo mjini Iringa wakati wa hafla ya kuhuisha na kusaini makubaliano mapya ya mgawanyo wa hisa za BVC kati ya Halmashauri ya Wilaya ya Iringa na serikali ya Kijiji cha Bomalang’ombe.
Akizungumza baada ya kusainiwa kwa makubaliano hayo, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, Robert Masunya, alisema pande hizo zimekubaliana rasmi modeli mpya ya ugawaji wa hisa ili kuweka utulivu, uwazi na uendelevu wa miradi inayosimamiwa na kampuni hiyo.
Kwa mujibu wa Masunya, Halmashauri ya Wilaya ya Iringa ndiyo mwenye hisa kubwa kwa asilimia 55.6, huku asilimia 44.4 zikigawanywa kati ya vijiji vya Bomalang’ombe na Lyamko.
Ameeleza kuwa miradi ya BVC ilikuwepo hata kabla ya halmashauri za Kilolo na Iringa kutenganishwa kimamlaka. Awali, wanahisa walikuwa ni Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, kampuni ya Kiitaliano CEFA, na Kijiji cha Bomalang’ombe.
Ameongeza kuwa makubaliano mapya yamelenga kuondoa sintofahamu iliyodumu kwa miaka mingi na kuweka msingi wa usimamizi bora wa rasilimali za kampuni hiyo kwa manufaa ya wananchi.
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: