RC Kheri James Aagiza Wazabuni Wakamatwe Kwa Kukwamisha Ukamilishaji Kituo cha Afya Iringa Vijijini
Автор: Focus TV Tanzania
Загружено: 2025-12-18
Просмотров: 208
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Kheri James, amekerwa na hali ya kusuasua kwa Ujenzi na Ukamilishaji wa Kituo cha Afya katika Kijiji na Kata ya Mahuninga Tarafa ya Idodi halmashauri ya Wilaya ya Iringa, ambapo ametoa Maelekezo huku akiagiza wakamatwe wale Wazabuni wanaokwamisha mradi huo uliotakiwa kukamilika na kuanza kutoa huduma za Afya miezi mitano iliyopita lakini mpaka Sasa umekwama katika hatua ya umaliziaji.
RC Kheri James ametoa Maelekezo na maagizo hiyo Desemba 18, 2025, katika Ziara yake ya Ukaguzi wa hali na hatua iliyofikiwa katika Ujenzi wa mradi wa Kituo hicho cha Afya.
Aidha, katika Ziara hiyo, RC Kheri James, amepata fursa ya kufanya Mkutano wa hadhara wa kuzungumza na Wananchi wa Kata ya Mahuninga pamoja na kusikiliza na kutatua kero na Changamoto zao zinazokwamisha shughuli zao na kuchelewesha Maendeleo.
Focus TV ni chombo cha habari cha mtandaoni kinachorusha Maudhui yanayohusu Habari, Mitindo ya Maisha, Utamaduni, Michezo na Burudani kwa kuyaongezea thamani kwa maslahi ya umma.
.................
Focus TV is one of the Best Online TV Conveying Content and adding values for the public interest.
Focus TV is here to provide you with contents covering News, Education, Lifestyles, Culture, Sports and Entertainments.
Focus TV imesalijiliwa Nchini Tanzania na kupewa Leseni ya kurusha maudhui mitandaoni kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).
Asante kwa kuchagua kutufuatilia | Thanks for Subscribing
We Love You | Tunakupenda
Regards
Team Focus TV Tanzania
#FocusTVTanzania
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: