ZIARA ya Kamati ya Siasa Mkoa wa Ruvuma , Wilayani Tunduru.
Автор: tunduru_dc
Загружено: 2023-10-08
Просмотров: 715
Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Ruvuma yampongeza Mkuu wa Mkoa na Serikali kwa utekelezaji wa miradi ya maendeleo Tunduru
Kamati ya Siasa ya Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Ruvuma imefanya ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo wilayani Tunduru, ikiwa ni pamoja na ujenzi wa Shule mpya, maabara, majengo ya Tehama, mabweni,na vyoo. Ziara hiyo iliongozwa na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa, Mhe. Komred Oddo Mwisho, na iliambatana na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Mhe. Kanali Labani Thomas.
Baada ya kukagua miradi hiyo, Kamati iliridhika na utekelezaji wake. Komred Mwisho aliipongeza Serikali ya Awamu ya Sita kwa kuendelea kutoa fedha za miradi ya maendeleo, na pia aliipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru kwa kusimamia vyema utekelezaji wa miradi hiyo. Alisema kuwa utekelezaji wa miradi hiyo umekuwa wa kuridhisha na unakwenda sambamba na maelekezo ya Serikali.
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: