KAMBI TEMBEZI YA MATIBABU BILA MALIPO YAZINDULIWA RASMI UKEREWE
Автор: aboodmedia tz
Загружено: 2025-11-18
Просмотров: 4
Serikali kupitia divisheni ya afya wilayani Ukerewe kwa kushirikiana na Canada African Community Health Alliance (CACHA) imeendelea kuwathamini wananchi kwa kuanzisha kambi tembezi ya matibabu bila malipo itakayofanyika kwa vituo tisa kuanzia Novemba 17 hadi 27, 2025 kwa magonjwa yote ya ndani,
Akizungumuza katika ufunguzi wa kambi hiyo uliofanyika katika kituo cha afya cha Igalla kilichopo kata ya Igalla Mkuu wa wilaya ya Ukerewe Cde, Christopher Ngubiagai amewataka wananchi kuupokea mpango huo wa serikali ili kuleta ustawi wa jamii ya Ukerewe.
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe Dkt. Charles Mkombe ameipongeza serikali kwa mpango huo madhubuti wa kuwapelekea wananchi huduma huku akisema kutakuwa na ongezeko la siku saba za upasuaji katika hospitali ya Wilaya Hiyo .
Nae daktari kiongozi wa kambi hiyo Bunhya Kayila amewasisitiza wananchi kuendelea kujitokeza katika vituo vyote vilivyoainishwa kwa ajili ya kupata matibabu hayo kwani timu ya madaktari ipo tayari kuwahudumia
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: