Shuhudia Uvunaji wa kwanza wa samaki wa vizimba, Kisoko Mkoani Mwanza tarehe 25/09/2024.
Автор: tadbtz
Загружено: 2025-02-18
Просмотров: 3713
Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) kwa kushirikiana na Wizara ya Mifugo na Uvuvi, imeshuhudia uvunaji wa kwanza wa samaki wa vizimba katika eneo la Kisoko, Mkoani Mwanza tarehe 25/09/2024.
Upandikizaji wa Samaki hao ulianza Februari 22, 2024 kwa vikundi 12 ambapo kikundi cha Vijana Nguvu Kazi kilikua cha kwanza kupandikiza vifaranga 90,720 katika vizimba vyao 9, samaki hao wanaovuliwa wana uzito wa kati ya gramu 500 hadi Kilo 1.2 na watauzwa kwa wastani wa TZS 8,000/= kwa kilo.
Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa kushirikiana na TADB inaendelea na utekelezaji wa programu ya utoaji wa mikopo ya masharti nafuu isiyo na riba ya pembejeo na zana ufugaji samaki kwa vizimba.
Programu ilizinduliwa rasmi tarehe 30.01.2024 na Rais wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ambapo wanufaika ni vikundi, vyama vya ushirika, makampuni na watu binafsi kutoka Kanda ya Ziwa. Hadi sasa vizimba 222 vya awamu ya kwanza vimepandikizwa vifaranga kwa awamu na sasa programu inaendelea katika Wilaya za Misungwi, Magu, Bunda, Rorya na Busega.
#KilimoKinaBenkika
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: