WAZIRI MKUU DKT. MWIGULU ALIVYOWASHITUKIA NA KUFICHUA SIRI USIYOIJUA YA WAKANDARASI / AWAWASHIA MOTO
Автор: KAHITILA 255
Загружено: 2025-12-17
Просмотров: 766
WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba amewaagiza Watendaji Wakuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) na Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) kufanya tathmini ya miradi yote ambayo malipo ya awali yameshafanyika na hatua za ujenzi zilizofikiwa katika miradi hiyo.
Pia amewaagiza kuangalia kama utekelezaji wa miradi hiyo unaendana na kiwango cha fedha ambacho kimeshatolewa. “Na ikiwa itapatikana miradi ambayo imefanyika chini ya fedha iliyopatikana itakuwa ni hujuma dhidi ya uchumi wa nchi yetu, hawa ni lazima wafike kwenye mkono wa sheria”.
Ametoa maagizo hayo leo, Jumatano, Desemba 17, 2025 wakati akizungumza na wananchi baada ya kukagua uharibifu wa miundombinu mbalimbali ikiwemo mzani wa. Magari (Mpemba), Mahakama ya Mwanzo Tunduma, soko la Machinga akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Songwe.
#kahitila255 #wazirimkuu #daressalaam #tanzania
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: