NZEGA MOTO UMEWAKA DC NAITAPWAKI ANG`AKA.
Автор: KIMM MEDIA
Загружено: 2025-04-09
Просмотров: 2448
Mkuu wa wilaya ya Nzega mkoani Tabora Naitapwaki Tukai ameiagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU wilayani humo kuchunguza na kuwachukulia hatua za kisheria waliohusika na ubadhilifu wa zaidi ya shilingi milioni 500 iliyopekwa kwa ajili ya ujenzi wa majengo 8 ya shule ya sekondari ya Kampala.
Kufuatia kusuasua kwa majengo 8 ya madarasa, bwalo la chakula na matundu ya choo ya shule ya sekondari Kampala Diwani wa Kata ya Ndala Ramadhan Nchimani akasimama na kuomba hatua za kisheria zichukuliwe dhidi ya wasimamizi wa mradi huo.
Aidha Mwenyekiti wa kamati ya Fedha ya Halmashauri ya wilaya ya Nzega Vijijini Kitondo Seleli na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Henerico Nhwangi wameitaka serikali kutuma timu ya uchunguzi kwenye ujenzi wa majengo ya sekondari ya Kampala katika Kata ya Ndala.
Baada ya sintofahamu hiyo Mkuu wa wilaya ya Nzega Naitapwaki Tukai ameiagiza TAKUKURU wilayani humo kuchunguza miradi yote ambayo inasuasua umaliziaji wake na watakao bainika na ubadhilifu wafikishwa kwenye vyombo vya sheria.
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: