Mutahi Kahiga Statement : Kifo cha Raila Amolo Odinga
Автор: Swahili Time
Загружено: 2025-10-21
Просмотров: 14
Gavana #Mutahi_Kahiga amejitokeza na kuanza kusherehekea kifo cha Kiongozi Mkuu wa Upinzani, Hayati Raila Odinga (Baba).
Waombolezaji na viongozi wengine wamemkashifu huku wakijiuliza iwapo gavana huyu anajua kesho yake ,na kama hajui anyamaze maana kesho yetu iko mikononi mwa Mungu. Gavana huyu ameonekana mtu asiye na utu na anastahili kukumbana na mkono wa Sheria huko kamiti.
Wakosoaji wengi wamemkumbusha Gavana Kahiga kwamba ni mapambano ya kihistoria ya Raila Odinga ndipo Ugawaji wa Madaraka (Devolution) kupatikana na ndio maana ameshikilia na kuhudumu kama Gavana wa sasa, vinginevyo angekuwa anafuga nguruwe huko geshagi. Vitendo vya Gavana Kahiga havitazamwi tu kama kukosa heshima, bali kama fedheha kubwa kwa tabia ya uongozi.
Tabia ya Gavana Kahiga imetajwa kuwa haikubaliki kabisa hata na shetani. Wito umetolewa kwamba Gavana Kahiga amedhalilisha ofisi anayoishikilia na anapaswa kuchukua hatua inayofaa kwa kujiuzulu mara moja. Kenya inastahili viongozi ambao wanatetea na kuonyesha heshima, huruma, na umoja wa kitaifa, hasa wakati huu mgumu ambapo taifa linaomboleza kuondoka kwa mmoja wa mashujaa wake wakubwa wa kisiasa na demokrasia. Una maoni gani ? Kwa habari zaidi usikose kutufuatilia hii ni swahili time Dunia darubini #swahilitime #news #habari
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: