JINSI YA KUPIKA CHAPATI ZA KAROTI
Автор: Meju Mapishini
Загружено: 2025-07-28
Просмотров: 85
MAHITAJI
Unga wa ngani vikombe 2
Karoti moja kubwa
Mafuta ya kupikia vijiko 2 vikubwa
Chumvi kijiko nusu kikubwa
MATAYARISHO
1. Changanya unga:
Weka unga kwenye bakuli, ongeza karoti,mafuta na chumvi kisha changanya vizuri.
2. Kanda donge:
Ongeza maji kidogo kidogo huku unakanda mpaka upate donge laini na lisiloshikana mikononi.
Mwisho, paka mafuta kidogo juu ya donge ili lisikauke.
Funika donge na ulilaze kwa dakika 5-10 hivi
3. Tengeneza miduara:
Gawa donge vipande vidogo sawa.
Kila kipande kizungushe kwa umbo la duara ukitumia unga kidogo ili lisishike.
4. Pika chapati:
Weka chapati kwenye Kikaango kilichopata moto..
Pika upande mmoja hadi uone madoa ya kahawia, kisha geuza upande wa pili.
Paka mafuta au samli juu yake, kisha ugeuze tena.
Fanya hivyo kwa upande mwingine pia hadi chapati iwe tayari.
Hatimaye zitakuwa tayari kwa maandalizi.
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: