WAZIRI AWESO ASHTUKIZA RUVU CHINI KUJIONEA HALI YA MAJI, APIGA KAMBI DAR "TUMEPATA ATHARI"
Автор: Millard Ayo
Загружено: 2025-12-07
Просмотров: 3187
Leo tarehe 7 Disemba 2025. Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso amefanya ziara ya kikazi kwa kutembelea mtambo wa uzalishaji maji wa Ruvu Chini na kujionea hali ilivyo, Ikiwa ni mwendelezo wa jitihada za Wizara ya Maji kupunguza changamoto ya upungufu wa huduma ya hiyo, uliojitokeza Mkoani Dar Es Salaam kutokana na kuchelewa kwa msimu wa mvua.
Aweso amewasihi wananchi kujenga utamaduni wa kutunza maji katika kipindi hiki cha uhaba pia ameitaka Mamlaka ya Majisafi na usafi wa mazingira (DAWASA) kushirikiana na wadau binafsi wenye visima vikubwa ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma.
Pia aweso ameongeza kwa kutoa maagizo kwa DAWASA kuhakikisha visima vyote vilivyochimbwa na serikali vinaingizwa kwenye mfumo ili kuongeza hali ya upakinaji wa maji Mkoani humo.
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: