Wahukumiwa kunyongwa kwa mauaji ya mfanyabiashara wa madini
Автор: UTV Tanzania
Загружено: 2025-06-23
Просмотров: 5790
Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imetoa hukumu ya kifo kwa kunyongwa dhidi ya askari wawili kati ya saba waliokuwa wanakabiliwa na kesi ya mauaji ya mfanyabiashara wa madini, marehemu Musa Hamisi, mkazi wa Nachingwea mkoani Lindi.
Hukumu hiyo imesomwa mkoani Mtwara na Jaji Hamidu Mwanga, baada ya kusikiliza ushahidi wa pande zote pamoja na vielelezo 19 vilivyowasilishwa mahakamani. Mahakama imejiridhisha kuwa Girlbert Kalanje na Charles Onyango walihusika moja kwa moja na mauaji hayo.
Tukio hili limeibua hisia mseto kuhusu matumizi ya nguvu na maadili ndani ya vyombo vya ulinzi na usalama na wengine wakiona hukumu hii kama hatua ya haki kwa familia ya marehemu.
#azamnewsupdates
✍John Kasembe
Mhariri| @official_jennifersumi
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: