SOMO: VITA KATIKA AKILI; Mnenaji: Apostle Daniel Stanslaus
Автор: Peniel Church Media
Загружено: 2025-10-05
Просмотров: 15
SOMO: VITA KATIKA AKILI
*Hosea 4:6
"Katika akili ya mtu Kuna mtazamo, kumbukumbu na mawazo."
Mtazamo ni namna/jinsi ambavyo mtu anavyochukulia jambo.
Kumbukumbu ni mchakato wa kurejesha mawazo yaliyopita.
Mawazo ni uwezo na namna ya kufanya maamuzi.
Ili shetani aweze kuyaharibu maisha yako vizuri, anaanzia katika ufahamu na Akili yako.
*Warumi 12:2
Kuna wakati adui huweza kukutengenezea mazingira ya kukufanya uyasahau/usiyajue kabisa makusudi ya MUNGU juu yako. Ndiyo maana wakati mwingine mtu huacha kuomba/kukaa karibu na MUNGU.
Mawazo mengine yasiyo ya kiMungu yanapoletwa akilini mwako,jifunze na jitahidi kuyanyamazisha! Yanyamazishe kwa NENO la MUNGU! Nyamazisha sauti zote zinazoingilia kuamini kwako juu ya MUNGU!
Mazingira magumu huweza kuja kwako; dhoruba, upepo mkali, na vitisho, lakini usiyaruhusu yakutoe katika kuyafahamu Yale mapenzi ya MUNGU juu yako.
*Kutoka 16:3, 32:1
Sisi ni wasafiri ambao MUNGU anatuhamisha Kutoka hatua moja kwenda nyingine. Akili zetu zinapokuwa nyuma kule tulipotoka, hatutoona mapenzi kamili ya MUNGU yakidhihirika maishani mwetu.
"_ihamishe akili Yako Kutoka huko nyuma na kuangalia mbele!_"
Hata pale ambapo BADO hujaona mpenyo katika yale unayomtegemea, usiyakumbuke mambo ya nyuma! Usiiache akili yako itazame nyuma! Kushindwa kwako kwa Jana haimaanishi utashindwa na kesho!
Ifanye akili yako kuwa mpya Kila siku, kwa Neno la MUNGU! Tunza akili na ufahamu wako!
Usipoitunza akili Yako,inaweza
ikakupelekea kufanya maamuzi ambayo yatakugharimu maisha yako yote!Usiruhusu mazingira yaamue maamuzi yako!
*Wafilipi 4:8
Unawaza Nini juu ya MUNGU, hata pale ambapo mambo mabaya yamekujia? Unamuwazia Nini MUNGU, pale magumu yanapokujia?
Usiwe mwamini wa kuyumbishwa-yumbishwa na upepo! Nafasi ya MUNGU katika maisha yako usiruhusu ikabadilishwa na mazingira!!
"_Isemeshe akili yako! Iambie ikatulie! Na ikamtazame MUNGU na AHADI zake!_"
*2 Korintho 10:5
Mwamini MUNGU mpaka dakika ya mwisho! Hata pale unapoona mambo hayajabadilika katika ulimwengu wa mwili, ila mwamini MUNGU tu!
_"tofautisha kati ya maneno ya watu na Neno la MUNGU, maana ni vitu
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: