INAYODHANIWA KUWA NDEGE YA KICHAWI YADONDOKEA JUU YA BATI MTWARA| WAHUSIKA WAILILIA KWA UCHUNGU
Автор: Faida Online TV
Загружено: 2025-07-18
Просмотров: 4046
Wananchi wanaoishi kwenye Mtaa wa Tandika Manispaa ya Mtwara Mikindani Mkoani Mtwara na wale wapita njia, mapema hii leo wamekusanyika kwenye moja ya Nyumba zilizopo kwenye Mtaa huo kushuhudia kitu kinachodhaniwa kuwa ni Ndege ya kichawi ambayo inasemekana ilinasa katika Nyumba hiyo ambayo ni eneo la kazi la Mtaalam mmoja yaani Mganga wa kienyeji.
Wakiongea na Faida Online tv Wapangaji wa Nyumba hiyo wanasema kitu hicho kilinasa usiku wa Manane ambapo mmoja wao alikiona kikiwa juu ya bati alipotoka nje kujisaidia na muda Mchache baadae walisikia watu wakirusha Mawe ili kukidondosha ila Kwa bahati mbaya hakikudondoka na ndipo alipofika Mtaalam anayefahya kazi hapo na kukishusha Kisha kukichoma moto.
Mtaalam huyo hakuwa tayari kuzungumzia kilichotokea huku akitumia nguvu kubwa kuwaondoa Wananchi katika eneo hilo.
Wananchi hao walianza kutawanyika mara tu baada ya kitu hicho kuchomwa moto mbele ya kilinge cha Mtaalam huyo na kuteketea moja kwa moja.
Kitu hicho kinachodhaniwa kuwa ni Ndege ya kichawi ni Nyungo ikiwa na miti, Chungu kidogo, na vifundo kadhaa.
#FaidaOnlinetvUPDATES
Tufuatilie kwenye mitandao yetu ya Kijamii,
YouTube Instagram na X 👉 Faida Online tv
Facebook 👉 Karim Faida
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: