POLISI MWANZA WATOA ELIMU YA USALAMA BARABARANI KWA BODABODA KUELEKEA UCHAGUZI MKUU
Автор: Kwizera TV
Загружено: 2025-10-24
Просмотров: 6
MWANZA: Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Mwanza, Mrakibu wa Polisi SP Sunday Ibrahim, leo ametoa elimu kwa madereva wa bodaboda mkoani humo kuhusu umuhimu wa kuheshimu misafara ya viongozi ili kuepusha vurugu na ajali barabarani.
Akizungumza katika kikao hicho cha elimu, SP Ibrahim amesisitiza kuwa ni muhimu kwa madereva wote wa bodaboda kutambua na kufuata kanuni za usalama barabarani, hasa wakati misafara ya viongozi inapopita, ili kuepusha migongano na kuchukua hatua sahihi kisheria.
Kwa upande wao, baadhi ya madereva walioshiriki mafunzo hayo wameeleza kuwa wamepata uelewa mkubwa na wako tayari kufuata sheria na kanuni hizo kwa manufaa ya usalama wao na watumiaji wengine wa barabara.
Na Fredy Seleli- Mwanza
_________________
Radio Kwizera Ngara Kagera Tanzania | Unaweza kuisikiliza Radio Kwizera kwa masafa mbalimbali: 97.7 KAGERA, MWANZA & GEITA | 93.7 KIGOMA | 89.5 SHINYANGA
Unaweza kusikiliza kwa njia ya mtandao kwa kubofya link hapo chini https://radiokwizera.co.tz/
LIKE | FOLLOW | SUBSCRIBE | COMMENT | SHARE
© All Rights Reserved to JRS Radio Kwizera 1995-2025
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: