Uza Kitajiri

Habari Tajiri,
Karibu kwenye channel ya Uza Kitajiri. Channel hii inadhumuni moja kuu na dhumuni hilo ni KUTAJIRISHA MAISHA YAKO.
Binafsi hatupendi umaskini na tuliamua kuwa hatupo tayari kuishi maisha ya kawaida wala hatupo tayari kukubaliana na hali tuliyokuwa nayo ya umasikini na uhaba. Hivyo tulianza safari yetu ya kuelekea kwenye maisha ya UTAJIRI NA UKWASI.

Bado hatujafikia lengo hilo ila tumeshapiga hatua kadhaa kutoka tulipokuwa kuufikia hapa tulipo. Tumekuwa tukijifunza na kugundua mambo mengi ambayo yanaweza wewe Tajiri Mwenzetu kutoka hapo ulio kuelekea kwenye yale maisha unayoyaona tu kwenye ndoto au fikra zako.

Jiunge nasi kwenye safari hii. Hii sio kwaajili ya kila mtu bali ni kwaajili ya wale wachache waliochoshwa na hali ya UMASIKINI, HABA, SHIDA au MAISHA YA KAWAIDA na sasa wanataka kufanya mabadiliko na kuanza kutembea kwenye maisha ya UTAJIRI, UKWASI, RAHA, na MAISHA YA UTOFAUTI.

Sisi ni MATAJIRI mwenzenu Ian, Kevin & Melekzedeck Metili.

Hakuna kisichowezekana.