"JITIHADA ZA RAIS ZINAIMARISHA SEKTA YA BIASHARA ZANZIBAR" WAZIRI HAMZA
Автор: ASAM Online TV
Загружено: 2026-01-17
Просмотров: 186
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Mhe. Hamza Hassan Juma, amesema jitihada za Rais wa Zanzibar zinaonekana wazi katika kuboresha sekta ya biashara, akizitaka wizara husika kuendelea kutunza na kuimarisha maeneo ya biashara ili kuwawezesha wafanyabiashara kufanya shughuli zao kwa ufanisi.
Ameyasema hayo wakati wa ufungaji wa Maonyesho ya 12 ya Mapinduzi ya Zanzibar yaliyofanyika katika Viwanja vya Dimani, Mkoa wa Mjini Magharibi.
Naye Dkt. Habiba Hassan Omar amesema maonyesho hayo yamelenga kuwakutanisha wafanyabiashara na wajasiriamali ili kujenga ushirikiano, kubadilishana uzoefu na kupata fursa za mitaji kupitia taasisi za kifedha. Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara, Ndugu Ali Amour, amesema mafanikio ya maonyesho hayo ni hatua muhimu katika kuwawezesha wafanyabiashara kujenga mitandao yenye tija.
#AsamOnlineTV #MapinduziZanzibar #SektaYaBiashara #Dimani #Wajasiriamali #MaendeleoEndelevu
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: