ZAIDI YA WATOTO ZAIDI YA 500 WAPATIWA MSAADA WA VIFAA VYA MASOMO - KASKAZINI UNGUJA
Автор: ASAM Online TV
Загружено: 2026-01-19
Просмотров: 324
Mwakilishi wa Jimbo la Kijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Zanzibar, Mhe. Badria Attai Masoud, amegawa vifaa vya masomo (stationery) kwa zaidi ya wanafunzi 500 wakiwemo mayatima na watoto wanaoishi katika mazingira magumu.
Hafla hiyo imefanyika katika Skuli ya Potoa, Wilaya ya Kaskazini A Unguja, ambapo Mhe. Badria amesema msaada huo umetokana na ufadhili uliopatikana kwa lengo la kuwawezesha watoto kusoma kwa mwaka mzima na kurejesha tabasamu lililopotea, ikiwa ni utekelezaji wa ahadi za kampeni za kutoa kipaumbele kwa elimu.
Ametoa shukrani kwa Taasisi ya Asalam Community Foundation kwa kuunga mkono jitihada hizo. Naye Katibu Mkuu wa taasisi hiyo, Ndugu Sadiki Mohammed Ali, amesema lengo lao ni kuwahamasisha na kurejesha imani kwa watoto mayatima na wanaoishi katika mazingira magumu pamoja na wazazi wao.
Kwa upande wao, wazazi na walezi wamepongeza uongozi wa shehia ya Kijiji pamoja na viongozi wao kwa jitihada zinazoleta manufaa kwa vizazi vyao. Imeelezwa kuwa baada ya zaidi ya miaka 8, hii ni mara ya kwanza taasisi hiyo kutoa vifaa vya masomo kwa wanafunzi wa Wilaya ya Kaskazini A Unguja.
#AsamOnlineTV #ElimuKwaWote #BadriaAttaiMasoud #KaskaziniUnguja #WatotoMayatima #AsalamFoundation #Zanzibar
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: