CCM MAHONDA WAHIMIZWA KUJIFUNZA KATIBA NA ITIKADI YA CHAMA
Автор: ASAM Online TV
Загружено: 2026-01-25
Просмотров: 120
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kaskazini Unguja, Ndugu Iddi Ali, amewataka wanachama wa Jimbo la Mahonda kujifunza Katiba ya CCM kupitia madarasa ya itikadi ili kufahamu wajibu wao na utekelezaji wa Ilani ya Chama.
Kauli hiyo imetolewa wakati wa uzinduzi wa Darasa la Itikadi Jimbo la Mahonda, lililolenga kuimarisha umoja na mshikamano miongoni mwa wanachama wa Chama cha Mapinduzi.
Amesema madarasa ya itikadi yatawasaidia wanachama kuelewa malengo ya CCM kwa wananchi na kuwataka kuwa tayari kuyadumisha na kuyaenzi kwa vitendo.
Kwa upande wake, Mjumbe wa Kamati ya Siasa Mkoa, Ndugu Pandu Salim Sungura, amewahimiza vijana kuwa na uzalendo, kushiriki madarasa ya itikadi na kujifunza wajibu wa kukilinda chama na taifa.
Naye Mjumbe wa Baraza Kuu Taifa na Mwanachama wa Jimbo la Mahonda, Ndugu Yusuf Tashmir Haji, amewataka vijana kushiriki kikamilifu katika madarasa hayo ili kujifunza historia ya nchi na misingi ya ujenzi wa taifa.
#AsamOnlineTV #CCM #ItikadiYaChama #KatibaYaCCM #Mahonda #KaskaziniUnguja #Uzalendo
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: