WARIDI WA BBC - HILDA NKABE, MAMA WA KIJANA WA MIAKA 18 MWENYE USONJI.
Автор: Lukiza Autism Foundation
Загружено: 2024-12-15
Просмотров: 838
Hilda Nkabe au Mama Lukiza ni Mama Mwenye Kijana mwenye Umri wa miaka 18 sasa ambaye ana Usonji. Kijana Huyu ajulikanaye kwa jina la Lukiza ndio chachu iliyopelekea kuanzishwa kwa Asasi ya Kijamii ya Lukiza Autism Foundation ambayo Hilda Nkabe ndio Mkurugenzi Mtendaji wake.
Siku ya Jumatano. Tarehe 11 mwezi wa 12 Mwaka 2024 Hilda Nkabe alihojiwa BBC Swahili kama Waridi wa BBC kuelezea maisha na safari yake ya kumlea Lukiza mpaka sasa akiwa na umri wa miaka 18.
Hilda ameelezea changamoto alizopitia ikiwemo unyanyapaa, dhana potofu kuhusu Usonji na gharama za Maisha kwa familia zenye watoto wenye Uhitaji maalum.
Aidha ameelezea vitu anavyojivunia ikiwemo watoto wake wawili, Taasisi ya Lukiza ikiwemo tuzo mbalimbali alizopata kwa harakati za kuielimisha jamii kuhusu Usonji na mabadiliko chanya yanayotokea kutokana na harakati hizi.
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: