TANROADS KUWEKA MIKAKATI YA KUHAKIKISHA MRADI WA IRINGA - KILOLO UNAKAMILIKA KWA WAKATI
Автор: Wizara ya Ujenzi
Загружено: 2024-07-10
Просмотров: 438
Kufuatia kuanza kwa kusua sua kwa utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa barabara ya kutoka Iringa hadi Kilolo yenye urefu wa kilometa 33.6, Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) imeingilia kati suala hilo na kuchukua hatua za makusudi ili kuhakikisha kasi ya utekelezaji wa mradi unaendana sawa na muda pamoja na mpango wa utekelezaji wa mradi huo ili kuhakikisha kwamba unakamilka kwa muda uliopangwa.
Moja ya hatua zilizochukuliwa na Wakala (TANROADS) nikukutana na kufanya kikao cha pamoja na mkandarasi anayetekeleza mradi huo kampuni ya China Henan Engineering company pamoja na mhandisi mshauri kampuni ya RV Associates kutoka nchini India na kisha kuweka mikakati ya pamoja ili utekelezaji wa mradi uendane sawa na mpango wa awali wa utekelezaji wa mradi huo.
Hayo yamesemwa Julai 09, 2024 na Mkurugenzi wa Miradi kutoka TANROADS Mhandisi Japherson Nnko alipotembelea mradi huo ambapo amesisitiza kuwa, moja ya sababu kubwa ya kuutembelea mradi huo ni kuona namna ya kuusukuma ili utekelezaji wake uende kwa kasi na haraka zaidi.
#wizarayaujenzi
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео mp4
-
Информация по загрузке: